Nina damu ndogo, nile nini kuongeza kiwango cha damu?

Tunapoenda hospitali na kugundulika na kiwango cha damu cha chini(Hb ndogo) huwa tunawaza tule nini ili kiwango cha damu kiweze kupanda na tuweze kuepuka athari zinazoweza kutokea.

Daktari Mkononi leo katika makala hii itakueleza juu ya aina ya vyakula unavyweza kula na kukuondoa wasiwasi wote juu ya hili.

Vyakula vinavyoweza kuongeza kiwango cha damu ni vyakula vile vinavyosaidia uzalishaji wa seli nyekundu, ukuaji wa seli hizi na hata utendaji kazi wake. Yapo makundi tofauti tofauti ya vyakula na hapa nitaweka katika mgawanyo wa jinsi vyakula hivyo vinavyofanya kazi kuongeza damu

1.Vyakula vyenye madini ya chuma

Hivi husaidia katika usafirishaji wa oksijeni katika mwili wa binadamu na pia ni sehemu kubwa ya seli nyekundu ya damu.

Mfano wa vyakula hivi ni nyama nyekundu, mboga za majani kama spinachi, maini, mayai na matunda kama beetroot

2.vyakula vyenye madini ya shaba

Hivi husaidia katika utendaji kazi wa seli nyekundu na katika utumikaji wa madini chuma yaliyopo kwenye seli.

Hii hupatikana kwenye nafaka, maharage, na hata jamii ya karanga.

3.Vyakula vyenye Folic acid

Hivi husaidia katika utengenezaji na uzalishaji wa seli nyekundu za damu.

Vyakula hivi ni kama mbogamboga, njerege ,maharage na jamii ya kunde.

4.vyakula vyenye Vitamin A

Hii husaidia ukuaji wa seli nyekundu ya damu.

Hivi ni kama karoti, matunda kama matikitimaji, mboga za majani, viazi vitamu.

5.Vyakula vyenye Vitamin B12

Vyakula vyenye hii nyama nyekundu, maziwa , siagi, mayai na samaki.

Usiruhusu tatizo la kuwa  na damu ndogo kukutawala , kula vyakula vya lishe na fanya mazoezi ili kuimarisha afya yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center