Fahamu Mambo Matano Muhimu Usioyajua Kuhusu Uke Wako

  1.  Uke hujisafisha  wenyewe:   huaminika usafi wa uke hutokana na kujisafisha na sabuni mbalimbali , viungo   na haswa maji ya moto. Ila ukweli ni kwamba uke unajisafisha wenywe  kwa utaratibu wake kutumia tezi na bakteria wanaolinda uke   . Uke unasafishwa na maji masafi tu tena  kutoka mbele kurudi nyuma.        
  2.   Kutokwa na  uchafu (ute) ni jambo la kawaida.Katika uke kutokwa na uchafu (Ute) ni suala la kawaida ,Haswa baada ya hedhi rangi ya ute unatakiwa uwe mwepesi, mweupe na unaovutika , usio na muwasho. Kama rangi ya njano,kijani, mwenye muwasho hio sio dalili nzuri  , Ni dalili ya magonjwa kama fangasi hivyo tembelea kituo cha afya haraka.   
  3.  Kila uke una harufu yake ya pekee:    Kila mwanamke ana harufu yake pekee ya uke  , Siku zote harufu hazifanani hata kidogo . Hii inatokana na aina ya vyakula tunavyokula, usafi  na utunzwaji wake, na jasho la mtu. Uke wa mwanamke hauhitaji manukato yoyote.
  4.  Kufanya mapenzi sana hakulegezi uke wa mtu : Dhana ya kwamba kufanya mapenzi sana kunalegeza uke wa mtu sio ya kweli. Ulegevu wa uke unatokana na kujifungua njia ya kawaida au swala la umri kwenda sana (uzee). Tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa kufanya mazoezi ya (kejels) yanayo saidia misuli ya uke iliyolegea kukaza.       
  5. Magonjwa ni kitu cha kawaida usiogope.  Magonjwa kama U.T.I , fangasi na muwasho sehemu za siri ni jambo la kawaida yasikutishe . Jambo la msingi hali isiyo ya kawaida ikitokea katika uke wako tembelea kituo cha afya mara moja ukaonane na daktari wa akina mama kwa matibabu Zaidi.

Irene Mtabo

Mental health is important.

All author posts

Privacy Preference Center