Fahamu kuhusu Chango kwa watoto

Utangulizi

 • CHANGO ni maumivu makali ya tumbo anayoyapata mtoto mdogo ambayo huambatana na kulia mara kwa mara zaidi ya masaa 3 kwa siku ,kwa zaidi siku 3 mfululizo, kwa muda wa wiki 3 na zaidi kwa mtoto ambae hana tatizo lolote la kiafya.
 • Hali hii hujitokeza mara nyingi kwa watoto wenye umri wa wiki 2, kwa baadhi hutokea zaidi ya muda huo na hali hii mara nyingi huendelea hadi pale mtoto anapofikisha miezi 3 mpaka 4
 • Mara nyingi watoto wengi hulia sana wakati wa jioni japokuwa inaweza kutokea wakati wowote na hivyo kusababisha hofu kubwa kwa wazazi au walezi wa mtoto na hata kupelekea msongo wa mawazo na pia kuhangaika kutafta huduma hospitalini au tiba mbadala mara kwa mara kwa kuhofia maisha ya mtoto wao.

Visababishi vya Chango

 • Mpaka leo hakuna kisababishi kinachojulikana kwa asilimia 100 kuwa ndio kinacholeta Chango kwa watoto.
 • Kwanza kabisa lazima tufahamu kuwa mfumo wa chakula wa mtoto mdogo unakua haujakomaa kama wa mtu mzima hivyo ni rahisi kwao kupata matatizo kwenye mfumo huu kirahisi

Zifuatazo ni baadhi ya sababu za chango

 1. Kumuanzishia mtoto maziwa tofauti nay a mama kabla ya kufikisha miezi 6. Maziwa ya ng’ombe ambayo yana protini nyingi ambazo ni ngumu kwa mtoto kuzimeng’enya huweza leta chango kwa watoto
 2. Kujaa kwa gesi tumboni ambayo mtoto huimeza anapolia au anaponyonya kama mama hatamuekea chuchu vizuri mdomoni hivyo kuruhusu mtoto kumeza hewa
 3. Maziwa ya formula ambayo yana Lactose ambayo yanaweza kumsababishia mtoto apate Allergy tumboni na kumsababishia maumivu ya tumbo
 4. Mtoto anaponyonya na kushiba kupita kiasi au kuvimbiwa ( overfeeding) pia husababisha chango

Huduma ya haraka kusaidia kutuliza Chango kwa mtoto

Njia hizi huweza punguza maumivu kwa mtoto

 1. Kumlaza mtoto kwa mgongo na hakikisha ni sehemu tulivu anayoweza kupumzika
 2. Unaweza kumlaza kwenye mapaja yako na kumsugua taratibu mgongo wake
 3. Njia nyingine ni kumweka kwenye maji ya uvuguvugu

Nifanye nini kumsaidia mtoto?

 1. Kwanza kabisa fika kituo cha afya cha karibu ili mtoto afanyiwe uchunguzi kuona kama hana tatizo jingine
 2. Epuka matumizi ya maziwa ya ng’ombe au ya formula kama hujashauriwa na daktari,kama hali inaendelea basi badilisha aina ya maziwa kulingana na ushauri wa daktari wako
 3. Mnyonyeshe mtoto ashibe kwa kiasi sio mpaka avimbiwe
 4. Hakikisha mtoto anapolia uweze kumnyamazisha mapema,asilie mda mrefu kwani kadri anavolia ndo anazidi kuongeza uwezekano wa kumeza hewa na kumuongezea maumivu.
 5. Hakikisha unapomnyonyesha mtoto chuchu inaingia yote mdomoni ili isiruhusu mtoto kumeza hewa, Kama ni chakula hakikisha unamlisha kidogokidogo mara kwa mara kuliko chakula kingi kwa mara moja

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.