Mambo 6 ya kustaajabisha usiyoyajua kuhusu uume (penis).

Inaposemwa mambo usiyoyafahamu kuhusiana na uume inaweza kuwa ni jambo la kufurahisha hasa kwa wanaume kwani uume ni rafiki wa karibu sana. Lakini hebu ungana nami tuangalie dondoo kadhaa za kustaajabisha kuhusiana na uume.

1.uume wa binadamu pekee hauna mfupa.

Uume wa binadamu unatofatiana na uume wa viumbe wengine kwani hauna mfupa bali umeundwa na misuli tu. Katika viumbe vingine mfupa husaidia uume kusimama lakini kwa binadamu haiko hivyo kwani uume kusimama kunatokana na damu kujaa kwenye misuli ya uume.

2. Uume huweza kuvunjika pia.

Pengine utajiuliza kama hauna mfupa sasa unawezaje kuvunjika? Lakini jambo hili linaweza kutokea kutoka na kufanya mapenzi kwa fujo, kupigwa na kitu au kuangukia uume ukiwa umesimama. Kuvunjika kunatokana na kuchanika kwa shithi (tunica albuginea shealth) ambayo huupatia uume ugumu pale unapodinda. Kuvunjika kwa uume husababisha maumivu makali na uume unakuwa hauwezi kusimama, upasuaji huhitajika kurekebisha tatizo hili.

3. Urefu sahihi wa uume ni zaidi ya ule unaonekana.

Unaweza usiamini lakini huo ndiyo ukweli wenyewe, wataalamu wanakadiria kuwa urefu halisi wa uume unaweza fika mara mbili ya urefu ule ambao tunaweza kuuona. Hii hutokana na ukweli kwamba misuli mingi ya uume imefichwa ndani ya mifupa ya nyonga hivo sehemu ya uume tunayoiona ni sehemu tu ya misuli hiyo, hivyo kufanya urefu halisi wa uume kuwa mkubwa kuliko ambavyo tunaweza kuuona.

4. Msisimko wa uume hupungua kadiri umri unavoongezeka.

Pamoja na uwepo wa kauli kuwa ng’ombe hazeeki maini, lakini tafiti zimeonesha kuwa kadiri umri unavyoongezeka ndivyo msisimko wa uume unavyopungua ingawa imekuwa vigumu kueleza moja kwa moja kuwa unapungua kwa kiasi gani kutokana na kutofautiana kwa njia ambazo zilitumika katika tafiti kusisimua uume.

5. Uume ni makazi ya vimelea pia.

Kama ilivyo kwa uke, pia ngozi ya uume ni makazi ya vimelea vya asili (normal flora) au vimelea vya maradhi (infectious micro-organism). Tafiti zimeonesha kuwa aina za vimelea hawa zinatofautiana kati ya mtu na mtu hasa kutokana na sababu kuwa hutegemana na hali ya usafi wa mtu binafsi, wale wasiokuwa na tabia ya usafi wa maeneo yao ya siri wana idadi kubwa ya vimelea hawa. Pia kutotahiriwa ni sababu ya kuwa na idadi kubwa ya vimelea hasa wale wanaoishi bila kutegemea hewa ya oksijeni (anaerobes) ikilinganishwa na wale waliotahiriwa.

6. Uume kusimama mara ya kwanza na kusimama mara ya mwisho.

Wengi wetu tunaweza kuwa tunafikiri ya kuwa mara ya Β kwanza uume kusimama labda ni wakati ulipoanza kujitambua wakati ukiwa bado na umri mdogo lakini ukweli hauko hivyo, tafiti zinaonyesha kuwa mtoto huanza kusimamisha uume toka akiwa akiwa katika mfuko wa uzazi (uterus). Lakini pia tafiti zinaonyesha kuwa mtu husimamisha mara mwisho pale anapofariki, hii hutokana na damu ambayo inakuwa iliingia kwenye misuli ya kushindwa kutoka baada ya muda mtu kufariki hivyo uume hubaki ukiwa katika hali ya kusimama, kusimama kwa aina hii mara nyingi hutokea kwa wale wanaofariki kwa kujinyonga.

Asante kwa muda wako kutembelea daktari mkononi naamini umefurahia dondoo hizi. Usisite kuuliza swali kwani timu ya daktari mkononi iko kwa ajili yako. Pia usisahau kushare.

10 thoughts on “Mambo 6 ya kustaajabisha usiyoyajua kuhusu uume (penis).

  1. Kuna mdada alishitakiwa kwa kosa la kufanya mapenzi na maiti… Wasn’t cling in my mind hahahah sasa nimeeleewa…..

    Asanteni sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center