FAHAMU JUU YA MAZOEZI YA KUIMARISHA MISULI YA NYONGA ZAKO (KEGEL EXERCISES)

Mwili wa binadamu una mifumo mingi ambapo mfumo wa Uzazi na mfumo wa utoaji takamwili kwa njia ya mkojo ni baadhi kati ya mifumo inayoingiliana katika ufanyaji wa kazi.

Mifumo hii miwili inahusisha ogani mbalimbali muhimu katika mwili wa binadamu kama;

聽聽聽聽聽聽聽聽 Kibofu cha mkojo

聽聽聽聽聽聽聽聽 Mfuko wa uzazi (mwanamke)

聽聽聽聽聽聽聽聽 Utumbo na

聽聽聽聽聽聽聽聽 Pulu (sehemu ya kutolea haja kubwa)

Ogani hizi kwa ujumla wake zinashikiliwa na kuwekwa katika sehemu zake husika na misuli iitwayo misuli ya nyonga(pelvic floor muscles)

Misuli ikikosa uimara wake nini kitatokea?

Misuli hii ya nyonga ikikosa nguvu baadhi ya mambo yanayoweza kutokea huwa ni ya aibu kama vile

聽聽聽聽聽聽聽聽 Kujikojolea

聽聽聽聽聽聽聽聽 Kupitisha hewa njia ya haja kubwa(kujamba)

聽聽聽聽聽聽聽聽 Kupitisha haja kubwa

Haya yote yanaweza tokea bila kusudi la mtu binafsi hivyo kumsababishia aibu.聽

Kitu kikubwa cha kuhofia endapo misuli hii imeishiwa nguvu ni pale itakaposhindwa kubeba/ kushikilia hizi ogani hivyo kusababisha ziweze kuanguka/kutoka nje kupitia matundu ya mwili kama vile kupitia uke kwa mwanamke au sehemu ya haja kubwa. Hali hii kitaalamu inaitwa Pelvic organ prolapse(POP).

Nini sababu za misuli hii kuishiwa nguvu?

Sababu zinazoweza sababisha POP zipo nyingi ila baadhi ni kama zifuatazo;

聽聽聽聽聽聽聽聽 Uzee

聽聽聽聽聽聽聽聽 Kubeba mimba

聽聽聽聽聽聽聽聽 Uzaaji wa njia ya kawaida kupitia uke

聽聽聽聽聽聽聽聽 Kufanyiwa operesheni sehemu za nyonga

聽聽聽聽聽聽聽聽 Kukohoa, kucheka, kupiga chafya kupita kiasi聽

Sasa haya mazoezi nawezaje kuyafanya?

Mazoezi haya ya misuli ya nyonga ni rahisi sana na hayahitaji kuwa na nguo za mazoezi au eneo. Ni mazoezi ambayo waweza kuyafanya hapohapo ulipo.

Ukiweza fanya yafuatayo utakuwa umeweza fanya haya mazoezi;

1.聽聽聽聽聽聽 Njia ya kwanza ni kuweza kubana njia ya haja kubwa bila kuhusisha misuli ya tumbo.

Hii inasaidia kuimarisha misuli inayozunguka tundu la haja kubwa, hivyo kuepusha kutoa hewa au kujinyea bila kukusudia wakati wa kucheka au kupiga chafya.

2.聽聽聽聽聽聽 Njia ya pili ni kuweza kuzuia mkojo mara nyingi uwezavyo kipindi unakojoa.聽Wakati wa kutoa haja ndogo, misuli hii huwa inasinyaa, hivyo basi kitendo cha kubana mkojo husaidia iweze kukaza ipasavyo.

Jambo kubwa la kufahamu ni kwamba,mazoezi haya waweza pia yapangia muda na sehemu, ambapo waweza kuyafanya kwa kufuata hatua zifuatazo;

聽聽聽聽聽聽聽聽 Lala chini (chali),

聽聽聽聽聽聽聽聽 Kunja miguu ,

聽聽聽聽聽聽聽聽 Nyanyua nyonga juu kisha,

聽聽聽聽聽聽聽聽 Bana njia ya haja kubwa na ndogo na kuachia kwa muda wa sekunde 3-5 , fanya mara nyingi uwezavyo.

Mwisho, Mazoezi haya unaweza聽 kufanya mahali popote, ukiwa unapiga mswaki, kuendesha gari, ukiwa unakula hata ukiwa unaangalia televisheni kwa sababu hufanywa ndani kwa ndani bila watu wanaokuzunguka kujua nini kinaendelea. Pia mazoezi haya ya umuhimu kwa wote wanaume na wanawake hasa waliotoka kuzaa. Kwa wanaume huweza pia kusaidia katika kuimarisha nguvu za kiume na pia kaharakisha uponaji wa wanaume wamefanyiwa operesheni ya tezi dume.

4 thoughts on “FAHAMU JUU YA MAZOEZI YA KUIMARISHA MISULI YA NYONGA ZAKO (KEGEL EXERCISES)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center