Je,umeridhika na mwanya wako?

Mwanya  ni nafasi katikati ya meno. Sehemu ambayo mara nyingi mwanya hutokea ni katikati ya meno ya mbele kwenye taya ya juu na inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 97 ya watoto wana  mwanya . kwa watoto ni kawaida na baadae katika ukuwaji wake mwanya huu huziba wenyewe. Kwa watoto wengine mwanya hubaki hadi ukubwani na mara nyingi ni kwasababu unakuwa wa kurithi (genetic) na unaweza kuta kwenye familia mama au baba anao pia.

Lakini pia mwanya huweza kusababishwa na vitu mbalimbali;

;

  • Ukubwa wa taya pamoja na meno. Watu wegine wana meno madogo ukilinganisha na taya na hivyo nafasi zinaweza kutokea na mara nyingi hutokea katikati ya meno ya mbele.
 
  • Kuwa na fizi nene kuliko kawaida. Fizi zinapokuwa kubwa zinasababisha meno kuwa mbalimbali na hivyo mwanya kutokea.
 
  • Ugonjwa wa fizi (gingivitis)ambao husababisha fizi kuvimba na baadae meno kulegea. Hii inasababishwa na usafi hafifu wa kinywa na hivyo kufanya meno kulegea na kutoka yenyewe kama ugonjwa ukiwa mkubwa zaidi(periodontitis). Meno yanapotoka yanasababisha meno mengine kusogea na baadae kupelekea mwanya.
 
  • Mwanya huweza kutokea pia kama nyuzi iliopo katikati ya meno ya juu ya mbele(labial frenulum) ni kubwa kuliko kawaida na hivyo kusogeza meno yale pembeni.
 
 

Kwa jamii zetu za kiafrika kuwa na mwanya ni urembo na wengi hupenda ubaki hivyo hivyo. Sio kila mtu lakini anaweza kuridhika na mwanya na wangependa kuuziba au kuupunguza. Kuna namna mbalimbali za kufanya hivyo kama ifuatavyo;

Njia ya kwanza ni kwa kuvaa waya maalum(braces) ambao una  uwezo wa kusogeza meno na kuziba mwanya

Njia ya pili ni kuweka material maalum (bondind and veneer) itakayoongeza ukubwa wa meno yale na kuziba mwanya kabisa

 

  •  Njia ya tatu ni kama mwanya umesababishwa na nyuzi katikati ya meno kuwa kubwa daktari wa meno anaweza kuipunguza na baadae kuuziba ule mwanya.
  •  Pia kwa mwanya unaosababishwa na magonjwa ya fizi,usafi mkubwa inabidi ufanyike ili kuhakikisha meno hayalegei tena.
"Kila mtu ana mtazamo wake kuhusu urembo na kila mtu ana haki ya kuonekanaanavyotaka yeye hivyo kama hujaridhika na mwanya wako usisite kumuona daktari wa kinywa na meno kwaajili ya ushauri na matibabu zaidi. Je wewe umeridhika na mwanya wako…TUAMBIE"

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center