Tatizo la usonji kwa watoto

Usonji ni nini

Usonji ni tatizo linaloathiri uwezo wa mtoto kuwasiliana na watu wengine, kujitenga na watu na kuwa na tabia za kujirudia rudia kitu mara nyingi. Mtoto huwa na tabia ya kipekee na kuonekana wa tofauti sana na wengine.

Tatizo hili haliishii utotoni tu bali huendelea hata ukubwani. Hlitibiki lakini watu hawa wana uwezo wa kutimiza ndoto zao kama wengine kwani huwa na uwezo wa kipekee katika kitu fulani kuliko vingine vyote.

Tafiti kutoka shirika la afya duniani (WHO), tatizo hili humpata mtoto mmoja kati ya watoto 160 duniani.

CHANZO CHA TATIZO HILI HAKIJAJULIKANA BADO LAKINI KUNA SABABU HATARISHI ZINAZOWEZA KUPELEKEA TATIZO HILI KAMA;
1. Mama kupata mtoto wa kwanza katika umri mkubwa yaani zaidi ya miaka 35.
2. Mama mjamzito kuwa na kisukari kipindi cha ujauzito.

DALILI ZAKE

Dalili za tatizo hili huonekana pale mtoto anapofikisha umri wa kuanza kuelewa na kuzungumza kama watoto wengine
1.Kushindwa kuzungumza maneno yanayoeleweka hivyo kushindwa kuelezea hisia zake au kitu anachokitaka na hivyo kusababisha kurudia rudia maneno.
2.Kushindwa kuonyesha ishara za kimwili za mawasiliano kama kupunga mkono, ishara za usoni (facial expression)
3. Kuwa mzito wa kuelewa mambo ukilinganisha na watoto wengine lakini pia huwa wana uelewa mkubwa kwa kitu fulani ambacho anakua na uwezo wa kukifanya kwa ufanisi wa hali ya juu.
Kuwa na michezo ya kujirudia rudia na kuchezea sehemu fulani ya kitu mara nyingi kuliko kawaida na wenzake, mfano kuchukua mda mwingi kupangilia vitu kama shilingi kwa mda mrefu.
4.Kujitenga na wenzake na hivyo kushindwa kijichanganya na kufurahia michezo, mazoezi na hata masomo na wenzake.
5.Kushindwa kuangalia watu usoni mda wa mazungumzo
6.Kuepuka kelele na sauti kwa kuziba masikio. Hii hutokana na kuathirika kwa jinsi akili inavyotuma na kupokea ujumbe kutoka kwenye milango ya fahamu.

Tatizo hili halina tiba ya moja kwa moja bali watoto hawa wana shule maalumu kwa ajili ya kuhudumia mapungufu yao katika mawasiliano, lugha na tabia.
Watoto hawa wana uwezo wa kutimiza ndoto zao kama watoto wengine endapo watawekwa katika mazingira ya kutotengwa, kupatiwa tiba kwa wataalamu wa afya ya akili pale inapohiyajika, mazoezi na mafunzo ambayo hupatikana katika vituo vya watoto wenye matatizo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center