Maambukizi ya sikio la kati (Otitis Media)

utangulizi

Maambukizi ya sikio la kati (Middle Ear) ni kati ya magonjwa mawili ya juu yanayosumbua sana watoto baada ya magonjwa ya Mfumo wa juu wa upumuaji (URTI)

• Kulingana na maumbile ya mrija (Eustachian tube) unaounganisha mifumo hii miwili husababisha watoto kupata maambukizi ya maskio kirahisi kuliko watu wazima. • Asilimia 90 ya watoto hupata maambukizi haya angalau mara moja kabla hawajavuka miaka mitano

Vitu vinavyopelekea kupata maambukizi ya sikio

1)Umri wa mtoto.maambukizi haya huwapata sana watoto chini ya miaka mitano sanasana
2)Mafua yasiyoisha,husababisha kuziba kwa mrija wa Eustachian na kusababisha kujaa kwa sikio la kati(Middle ear) hivyo kuongeza uwezekano wa wadudu kujaa na kuleta maambukizi ya sikio
3)Kunyonyesha kwa chupa 4)Mlundikano wa watoto mfano.Shule za awali huongeza maambukizi kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine 5)Watoto wenye magonjwa ya kuzaliwa mfano.Downs syndrome,Ukimwi ,kisukari

Dalili zake ni zipi?

1)Maumivu ya maskio 2)Kupungua kwa usikivu wa mtoto,mzazi anaweza kuona mtoto anasikia mpaka upaze sauti kidogo,anakasirika kirahisi 3)Kizunguzungu na maumivu ya kichwa 4)Mtoto anaweza kuwa na homa na hata kupunguza hamu ya kula 5)Majimaji kutoka kwenye maskio,hii ni hatua ya baadae kabisa kama mtoto atakuwa na maambukizi makali au yanayojirudia bila kupona

Jinsi ya kujikinga

1)Usafi kitu cha muhimu kuzingatia 2)Kupunguza matumizi ya chupa kwa ajili ya kunyonyesha 3)Epuka vitu vinavyomletea mwanao madhara ya allergy mf.vumbi,baadhi ya vyakula

Nini cha kufanya

1)Kuwahi kituo cha afya.daktari atafanya uchunguzi wa maskio,mdomo na pua kuangalia dalili zozote zinazoweza kuleta shida kwenye maskio 2)Bakteria ndio wanaongoza kusababisha maambukizi haya hivyo antibiotics hufanya kazi vizuri 3)Dawa za kupunguza maumivu n.k

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center