Skizofrenia ( Schizophrenia) ni nini?

Schizophrenia Kwa kiswahili ni Skizofrenia au Dhiki.

Ni ugonjwa wa akili ambao huathiri mtu anavyofikiria , anavyohisi  na anavyotenda.

Ugonjwa huu huonyesha kuwa na dalili za njozi (hallucinations) na imani za uwongo  (delusion) na pia shida katika utambuzi.

Dalili

Watu wenye skizofrenia inabidii wategeme wengine kwasababu wanashindwa kufanya kazi au kujitunza wenye vizuri.

Wengi wao pia huweza kataa matibabu na kubisha hawana shida yoyote.

Madhara ya ugonjwa huu huarthri familia, marafiki na jamii pia wanaomzunguka mgonjwa wa  skizofrenia.

Dalili za ugonjwa wa schizofrenia hubadilika kutegemeana na mtu.

Dalili hizi zipo katika makundi makuu manne.

Dalili za hakika (Postive symptoms)

Mfano  kama njozi na imani za uwongo.

Dalili za ukosekanaji  (Negative symptoms).

Ni vitu vilivyochukuliwa kutoka kwa mtu/mgonjwa

Mfano: Kushindwa  kuonyesha nyuso asilia (facial expression). Kukosa hamu ya kufanya kitu.

Dalili za utambuzi.

Huarthri jinsi mtu anavyofikiria.mfano kushindwa kuwa makini  .

Dalili za mhemuko.

Kukosa kuonyesha hisia.

Dalili kuu ni

Dhiki .

Kusikia sauti au kuona vitu,  kuhisi,  kuonja au kunusa vitu ambavyo havipo .

Imani za uwongo.

Imani kuwa wengine wanataka kuwaongoza au kufikiria kuwa wana nguvu au uwezo uliopitiliza.

Shida katika fikra.

-Kuruka kutoka mada moja kwenda nyiengine.

Dalili zingine

  • Kukosa hamasa katika kazi za kila siku.
  • Kushindwa kuelezea hisia zake .
  • Kujitenga na jamii ( Huku huamini mtu katika jamii anataka kuumumiza)
  • Shida katika kupangilia maisha ya kila siku.

Vihatarishi.

  •  Kurithi
  • Mazingira.
  • Kemikali kutokuihana kwenye ubongo.
  • Utumiaji wa madawa ya kulevya

Matibabu.

Hamna tiba kamili ya skizofrenia.bali matibabu husaidia kuupunguza dalili .

Na dalili hizi huwa maishani mwote wa mgonjwa huyo.

Matibabu yakifatiliwa mgonjwa anaweza ishi maisha ya kawaida.

Matibabu ni dawa na ushauri .

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center