Mimba zinazoharibika kutokana na magonjwa ya mifugo! (Part 1)

Nini maana ya Ugonjwa wa kutupa mimba (Brucellosis) ?

Ni ugonjwa wa kuambukiza ambao hukaa na hushambulia kizazi na hupelekea kutoa mimba na kusabisha kutopata mtoto kabisa (Ugumba); brucellosis hutoka kwa wanyama haswa ng’ombe na huenda kwa binadamu kwa kunywa maziwa, kula nyama, kunywa au kushika damu ya ng’ombe, kuvuta hewa chafu ambayo ina bacteria hao, maji ya chupa ya uzazi na kondo la nyuma la ng’ombe yenye vimelea vya ugonjwa huo. Pia binadamu anaweza pata kutoka kwa binadamu mwingne aliye athirika na ugonjwa huu. Brucella husababishwa na bakteria aitwaye brucella arbotus. Ila hadi sasa tunaaina nne ya vimelea hizi; Brucella melitensis (kutoka kwa kondoo; kali sana), Brucella suis (kutoka kwa nguruwe;kali sana), Brucella abortus (kutoka waka ng’ombe; siyokali/saizi ya kati),na Brucella canis (kutoka  kwa mbwa; saizi ya kati).

Je ugonjwa wa kutupa/kuharibu mimba (Brucellosis) huambukizwaje?

Kwa kuwa bakteria wa ugonjwa huu huishi kwenye sehemu ya majimaji (ugirigiri) ya mwili wa mnyama au tisu kama vile damu, nyama, maziwa, maji ya chupa ya uzazi na kondo la nyuma. kwahiyo wanyama hupata kwa kula au kugusa majani yenye kinyesi cha mnyama mgonjwa au masalia ambayo yanavimelea vya ugonjwa huu, kumlamba au kumgusa mdama,  pia kipindi wanyama wakiwa kwenye joto na kukutana na madume hupelekea kupata ugonjwa huu pia. Binadamu hupata kwa kunywa maziwa, kula nyama, kumshika mdama aliye zaliwa mda mchache,  kunywa au kushika kinyesi au damu ya ng’ombe, kuvuta hewa chafu ambayo ina bacteria, maji ya chupa ya uzazi na kondo la nyuma la mnyama mwenye vimelea vya ugonjwa huu.

Je ugonjwa wa kutupa mimba (brucellosis) unaweza mpata nani?

Ugonjwa wa kutupa mimba huwapata wanyama wanyonyeshao ama walio katika kundi la mamalia endapo watapata bakteria wa ugonjwa huu kupitia njia mbalimblai. Hii ina maana kwamba ugonjwa wa kutupa mimba (Brucellosis) unaambukiza binadamu, wanyama wafugwao kama vile; ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, farasi, mbwa, ngamia na pia wanyama pori kam mbwa mwitu n.k. Ng’ombe na mbuzi ni wanyama ambao huchochea na huchangia sana maambukizi ya ugonjwa hatari wa kutupa mimba kwa binadamu kuliko wanyama wengine. Ugonjwa wa kutupa mimba (Brucellosis) kwa binadamu usiposhughulikiwa mapema husababisha kifo.

Je ni kundi lipi walio hatarini  sana kupatwa ugonjwa huu?

Watu wote wanaweza patwa na ugonjwa huu endapo wata kula, kunywa, kugusa vimelea hivyo, na zaidi hata kujamiana na wenza wao walio ugua ugonjwa huo. Ila walio katika hatari zaidi ni madaktari wa mifugo, wapenzi wa maziwa, jibini la nyumbani, wapenzi wa nyama, wakulima, wachinjaji, wafanyakazi kushiriki katika usindikaji wa pamba ya wanyama.

Ni zipi dalili za ugonjwa wa kutupa mimba?

 1. Kwa binadamu

Kwa bahati mbaya na hatari zaidi binadamu wanaokumbwa na ugonjwa huu hudhani ya kuwa wanaugua malaria ama taifodi kwa kuwa hupata homa kali, kuumwa kichwa na na wengine hupatwa na maumivu ya tumbo. Ila ugonjwa huu hauponi kwa dawa zitumikazo kutibu malaria ama taifodi na mgonjwa hutibiwa mara kwa mara pasipo kupona kama ilivyo kawaida. Baadhi ya dalili hizo ni kama vile:-

 • Kupata homa za mara kwa mara/ vipindi.
 • Kichwa kuuma sana mara kwa mara
 • kupoteza uzito na afya kudhoofika
 • kutupa mimba ya miezi mitatu kwa wanawake.
 • maumivu katika viungo na hisia ya matatizo ya misuli
 • kupatwa na uchovu wa mara kwa mara
 • kupoteza hamu ya kula
 • ugonjwa na uvimbe wa viungo
 • kutokwa na jasho jingi
 • kuvimba kwa tezi

Dalili zipi tunaweza ziona kwa wanyama?

Zifuatazo ni baadhi ya dalili zinaoaweza onekana kwa wanyama:-

 • Kuvimba viungo vya mwili hasa miguu
 • Kutoa mimba haswa za miezi mitatu ya mwisho
 • Kuwa na homa
 • Kukosa hamu ya chakula na kudhoofika
 • Kubaki kwa mda mrefu na kondo lanyuma.
 • Dume kuvimba kende na viungo vya miguu
 • Ndama kuzaliwa wakiwa wamedhoofika

Je ugonjwa wa kutupa mimba kwa binadamu waweza kutambuliwa hospitalini?

Ugonjwa huu huweza kugunduliwa hospitalini na daktari kwa kutumia dalili na kwa kuchukua sampuli kwa binadamu kama vile damu, mkojo, baili, mafuta ya mfupa au majimaji ya mgonjwa na kupelekwa maabara kwa matokeo zaidi.

*Usikose toleo lijalo (Part two) juu ya  Madhara, tiba, njia na tahadhari ya kujizuia na kujikinga na ugonjwa huu*

Asante

38 thoughts on “Mimba zinazoharibika kutokana na magonjwa ya mifugo! (Part 1)

 1. Hakika jamii yapaswa kuelemishwa kuhusu Magonjwa haya hatarishi sababu wengi hawana uelewa kuhusu haya lakni wamekuwa katika mazingira hatarishi sana pasipo kujua…Kazi nzuri Dr. Nkwambi
  Isaya

 2. Ur really doctor bro keep it up I know soon ur going to be wonderful Dr only just work hard every thing is possible in forensic science we all ways believe that “Everything changes with the passage of time. In other word, there is nothi
  ng permanent and invariable ” Law of progressive change. I loved ur idea, knowledge and skills you have. Kaza jembe langu tutatoka tu

 3. Big up doctor…. We are together in educating our societies about different zoonotic diseases. It’s my hope that even medical doctors will join the idea as per public health situation in general….. Together Dr

 4. mafundisho mazuriii asa kwa mama zetu,kwahiyoo nategemea Lazima tujifunze na tuelimike asa utumiaji mkubwa wa nyama.

 5. Great job doctor, hope utaendelea kutoa kaz nzur za kuelimisha jamii juu ya magonjwa haya kwan ni hatar sana kwa binadamu na wanyama pia. Nikutakie kazi njema.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center