Dalili hatari za kuzifahamu wakati wa Ujauzito

Dalili hatari wakati wa ujauzito

"Uchungu wa mwana aujuae mzazi"

Ujauzito ni kipindi kigumu kwani kinahusisha mabadiliko mengi mwilini na hivyo huja na dalili mbalimbali kama vile kichefuchefu, kutapika mara kwa mara, kutaka kula aina fulani ya chakula na nyingine nyingi.

"Lakini kuna baadhi ya dalili ambazo zikionekana wakati wa ujauzito zinahitaji msaada wa haraka wa kimatibabu"
Hivyo ni vyema kuzifahamu na kujua hatua za kuchukua endapo zikitokea.

kutokwa damu

Kutokwa damu sehemu za siri wakati wa ujauzito ni kati ya dalili ya hatari kwani huweza fanya mama au mtoto aliye tumboni kupoteza maisha, hasa pale ambapo huambatana na maumivu ya tumbo.

kutokwa na ute wenye harufu mbaya

Kutokwa na ute ute wenye harufu mbaya sehemu za siri wakati wa ujauzito huwezaย  kuonesha maambukizi ambayo yanaweza pelekea kupoteza mimba kama hakutakuwa na matibabu ya haraka.

Kuvunjika kwa chupa kabla ya uchungu

Hii ni moja ya dalili kuwa inawezekana upo au yupo katika hatari ya kupoteza mimba.

uchungu kabla ya miezi tisa kufika

Kitaalamu hufahamika kama premature labour ambapo unaanza sikia uchungu kabla ya miezi tisa au wiki 36 kufika hii ni dalili ya hatari na ni vyema kuwahi hospitali au kituo cha afya mapema.

mtoto kuacha kucheza tumboni

Endapo umeanza/ameanza kusikia kupungua au kuacha kucheza kwa mtoto tumboni zaidi ya siku moja ni vyema ukawahi/kumuwahisha hospitali kwa uchunguzi zaidi.

presha kubwa

Kuwa na presha wakati wa ujauzito ambayo ni kubwa kuliko ya kawaida hii huweza pelekea kifafa cha mimba(Eclampsia) hivyo ni vyema kufanyiwa/akafanyiwa uchunguzi na vipimo mara kwa mara.

Kupoteza fahamu au kupata kifafa

Kupoteza fahamu na kushindwa kupata fahamu baada ya dakika chache wakati wa ujauzito pamoja na kupata kifafa ni kati ya dalili ambazo sio za kudharauliwa na hivyo ni vyema kuwahi kituo cha Afya au Hospitali mapema.ย 

ufanye nini ikiwa dalili mojawapo imetokea

Ni vyema kuwahi/kumuwahisha katika kituo cha Afya haraka na mapema kwani kuendela kuchelewa kunaogeza uwezekano wa kumpoteza mama pamoja na mtoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center