Maswali na majibu kuhusu saratani ya sehemu ya kwanza ya koo(Nasopharyngeal carcinoma)

Swali: Saratani ya sehemu ya kwanza ya koo ni nini?

Jibu: Saratani ya sehemu ya kwanza ya koo ni ugonjwa unaotokea katika sehemu ya kwanza ya koo ambayo huitwa nasopharynx.Sehemu hii ya mwili hupatikana kichwani na inaunganisha mfumo wa mtu wa chakula na hewa,kitaalamu nasopharynx au sehemu ya kwanza ya koo uunganisha hasa sehemu ya kwanza ya mfumo wa upumuaji wa mtu ambao huunganishwa moja kwa moja na matundu ya pua na sehemu ya juu ya mfumo wa hewa koromeo ambao upeleka hewa katika mapafu

Swali: Ni nini husababisha ugonjwa huo?

Jibu: Wanasayansi hawajatoa jibu la moja kwa moja ya kua ni nini usababisha saratani hii bali kama ilivyo saratani nyingine imebainika kwamba saratani ya sehemu ya kwanza ya koo hutokana na sababu zinazo husishwa na ugonjwa huo au huitwa risk factors,ambazo ni: β€’ Maambukizi ya virusi aina ya Epstein barr na Human papilloma , namna ambavyo virusi hawa huleta saratani hii bado ni swala lililo katika tafiti lakini kama ilivyo bainika kwa waathirika wengi wa saratani hii walishawahi kupata maabukizi ya virusi hivyo na kwa asilimia kubwa majibu ya maabara kwa wagojnjwa hawa imeonesha uwepo wa vinasaba vya virusi hivi. β€’ Uvutaji wa sigara kwa muda mrefu. β€’ Unywaji wa pombe kupita kiasi. β€’ Kufanya kazi katika maaeneo yenye vumbi la mbao au kwenye viwanda vya mbao kwa muda mrefu. Hizo ni kati tu ya baadhi ya vitu vinavyo husishwa na saratani hii.

Swali: Je kuna sababu zozote za kigenetiki au za kikanda zinazo saababisha saratani hii?

Jibu: Ndio.Wanasayansi wamethibitisha kwamba kuna uwezekano wa urithishwaji wa vinasaba kutoka kizazi kimoja kwenda kingine ambapo vinasaba hivyo vina waweka watu katika athari ya kupata saratani hii,mfano ilionekana kwamba familia au jamii ya watu wenye saratani hii ama ni babu au bibi,au mama au baba, watoto wao wako katika hatari kubwa ya kupata saratani Katika swala la kikanda imebainika kuwa jamii fulani ziko katika hatari kubwa ya kupata saratani hii mfano watu wa Asia na Japani,watu wa Afrika hasa Afrika magharibi.Lakini hii haijaleta maana kwamba watu hao tu ndio wanapata saratani hii la hasha! Mtu yeyote mahala popote anauwezekano wa kupata saratani hii kama yuko katika hatari ya kuipata

Swali: Je kuna uhusiano wa ulaji wa vyakula mbalimbali na saratani hii?

Jibu: Ndio. Imeonekana kwamba kwa jamii zinazo tumia samaki ama nyama iliyotunzwa kwa chumvi nyingi au samaki na nyama iliyotunzwa kwa moshi kama vile jamii za Asia wanavyo fanya basi wako katika hatari ya kupata saratani hii baada ya mtumizi ya muda mrefu wa vyakula hivo.

Swali: Ni nini dalili za mtu mwenye saratani hii?

Jibu: Dalili za mtu mwenye saratani hii ni kama zifuatavyo, na nyingi ya dalalili hizi zinatokana na kuanza kukosekana kwa ufanyaji kazi wa sehemu hii ya koo; β€’ Kuwepo kwa uvimbe katika shingo. β€’ Kushindwa kuona vizuri au uoni hafifu. β€’ Kupata maabukizi ya sikio yanayo jirudia recurrent ear infections β€’ Maumivu ya usoni au kuhisi ganzi usoni. β€’ Maumivu ya kichwa. β€’ Kuanza kupoteza uwezo wa kusikia au kusikia kama kelele a kengele masikioni kwa muda mrefu. β€’ Kushindwa kufungua mdomo. β€’ Kutoka damu puani. β€’ Vidodonda vya kooni. Ikumbukwe kua dalili hizi ni lazima ziwe kwa muda mrefu kwa mgonjwa .Na pia baadhi ya magonjwa yanakua yana dalili kama hizi basi ni vema kwenda kituo cha afya mapema kwa uchunguzi zaidi uonapo dalili kama hizi

Swali: Je kuna matibabu ya saratani hii?

Jibu: Mgonjwa anapo gundulika na saratani mara nyingi matibabu huanzishwa kutokana na hatua gani ya saratani imefikiwa,ukubwa wa uvimbe na afya ya mgonjwa mwenyewe.Mara nyingi matibabu yanakua ni ya mionzi ama madawa,kama baadhi ya saratani.Ni vema kufanya uchunguzi mapema wa sehemu ya shingo,pua na masikio ili kugundua mapema saratani hii,kwani uchunguzi wa awali na mapema huleta matokeo mazuri katika matibabu ya saratani hii. Karibu kwa maswali zaidi katika uwanja wa kutolea maoni hapa chini.Usisite kutoa maoni,ushauri na sisi tutafanyia kazi, karibu tena dakatari mkononi kwa Makala zaidi za afya ,tupe sapoti yako kwa kuwashirikisha jamii na marafiki!

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center