Je! Inawezekana Mimba Kutungwa Nje ya Mfuko wa Uzazi?( Ectopic Pregnancy)

       Ndugu msomaji, ni kweli kabisa!!. Mimba inaweza kutungwa nje ya mfuko wa uzazi.Katika hali ya kawaida, yai lililopevuka husafiri kutoka kwenye ovari(sehemu ambayo mayai ya mwanamke huzalishwa) na kupita ndani ya mirija ya fallopiani  ambamo yai hurutubishwa na na mbegu za kiume kuunda kiinitete ambacho husafiri hadi kwenye kuta za mfuko wa uzazi na kujishikiza huko.Sababu zozote zinazozuia kiinitete kushindwa kusafiri vizuri, kufika na kujishikiza katika kuta za ndani ya mfuko wa uzazi hupelekea mimba kutungwa nje ya mfuko wa uzazi.

   Zaidi ya asilimia 95% ya mimba zinazotungwa nje ya mfuko wa uzazi huwa katika mirija ya fallopiani (Tubal pregnancies) na kwa asilimia zinazobakia mimba inaweza kutungwa tumboni, kwenye ovari na hata kwenye mlango wa uzazi (cervix).Mimba zilizo nje ya mfuko wa uzazi huwa hazina uwezo wa kukua na kuwa mtoto kamili, mara nyingi husababisha mishipa ya damu iliyopo karibu kupasuka na hivyo damu huvuja ndani au nje ya mwili.Mimba hizi huchoropoka(ruptures) kutoka mahali zilipo jishikiza na kusababisha upotevu wa damu nyingi, maumivu makali na hivyo kitoto hupoteza uhai!

 •      VISABABISHI VYA MIMBA         KUTUNGA NJE YA MFUKO WA UZAZI 
 • Uvimbe au maambukizi ndani ya mirija ya fallopiani yanayoweza kuzuia kiinitete kusafiri na kufika katika mfuko wa uzazi.
 • Maambukizi ndani ya mfuko wa uzazi yanayo ondoa mazingira rafiki ya utungwaji wa mimba wa kawaida.
 • Kovu lililobakia baada ya upasuaji, hasa ule wa mfumo wa uzazi linalosababisha kiinitete au yai kukwama na kushindwa kufika katika mfuko wa uzazi.
 • Ukuaji usio wa kawaida(abnormal growth) na matatizo yanayojitokeza wakati wa kuzaliwa(birth defects) husababisha kuwepo kwa mirija ya fallopiani isiyo na umbo sahihi linalokwamisha usafirishaji wa yai au kiinitete hadi kwenye mfuko wa uzazi
 • JE!, NI NANI YUKO HATARINI?
 • Mama mjamzito mwenye umri wa miaka 35-44
 • Ikiwa mama mjamzito aliwahi kupata tatizo la kutungwa kwa mimba nje ya mfuko wa uzazi hapo kabla
 • Ikiwa alifanyiwa upasuaji wa tumbo au mfumo wa uzazi kwa ujumla wake.
 • Mama mjamzito mwenye ugonjwa au maambukizi katika mfuko wa uzazi( Pelvic Inflammatory Diseases), na uvimbe katika kuta za mfuko wa uzazi; Endometriosis
 • Mama mjamzito aliye wahi kutoa mimba mara kadhaa hapo kabla.
 • Mama mjamzito aliye wahi kutumia dawa za kuondoa ugumba 
 • Mama mjamzito anayevuta sigara , sigara huwa na kemikali iitwayo nikotini ambayo husababisha mirija ya fallopiani kuwa mwembamba.

                DALILI ZAKE
(a)Maumivu makali na yanayokuja na kutoweka yenye ukali unaotofautiana. maumivu haya huwa kiunoni,tumboni,mabegani na hata shingoni.
(b)kuvuja damu ukeni wakati wa ujauzito, damu inaweza kuwa kidogo au kwa wingi, hivyo hutegemeana na uzito wa tatizo
(c) uchovu, kizunguzungu na kuzimia

 

Picha: Zaidi ya asilimia 95% za mimba nje ya mfuko wa uzazi huwa ndani ya mirija ya fallopiani kama inavyoonekana katika picha hii.Uzito wa mtoto huelemea mirija hii na hivyo mimba huchoropoka na damu nyingi hpotea na hata husababisha kifo kwa mama na mtoto.

            MATIBABU

Matibabu ya mimba iliyotungwa nje ya mfuko wa uzazi yanaweza kuhusisha dawa maalumu inayopatikana hospitali.Pia upasuaji hufanyika ili kunusuru maisha ya mama mjamzito kama sehemu nyeti sana ya tiba.

Picha : mimba nje ya mfuko wa uzazi

          USHAURI 
Ni vyema kutembelea vituo vya kliniki mara kwa mara ili kugundua mimba zisizo za kawaida, mara nyingi ni vigumu kujua kama mimba imetunga nje ya mfuko wa uzazi kwa kutumia dalili peke yake.Pia mama mjamzito aepukane na uvutaji wa sigara na hata kujihusisha na utoaji wa mimba katika maisha yake 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center