Kwanini sifanyi mazoezi!? Naweza badilika!?

Karibuni sana wasomaji wa makala zetu za Daktari Mkononi katika kipengele chetu cha lishe na mazoezi. Siku ya leo tunazungumzia sababu kubwa ambazo hufanya watu kuto kupendelea kufanya mazoezi na vile vile kutoa baadhi tu ya njia ambazo mtu anaweza kuzifuata na kuweza kubadilisha tabia. 

Kwa kuanzia, kuna aina nyingi za mazoezi, baadhi yapo katika makundi yafuatayo;

1.       Mazoezi ya uvumilivu/endurance (aerobic) amabayo uhusisha mazoezi kama, kukimbia, kucheza mziki, kutembea na pia kuendesha baiskeli.

2.       Mazoezi ya nguvu ambayo mfano mzuri ni mazoezi ya kunyanyua vitu vizito.

3.       Mazoezi ya kujinyoosha mfano unyooshaji wa viungo wa kawaida na pia yoga

 

4.       Mazoezi ya kuimarisha balansi na stamina kama kusimama kwa mguu mmoja au kutembelea vidole.

Mazoezi tajwa yana umuhimu mkubwa sana kwa mwili wa binadamu. Faida kubwa za mazoezi ni kama kuimarisha mfumo wa mzungo wa damu kuanzia kwenye pampu ya damu (moyo) mpaka kwenye mishipa ya damu na kusaidia ogani mbalimbali ikiwemo ubongo kuweza kupata damu kwa kiwango sahihi ili kuweza endelea na kazi zake. Pia husaidia katika kuimarisha kinga za mwili hivyo kusaidia mwili kutoshambuliwa na magonjwa kwa urahisi. Kwa maelezo zaidi juu ya faida za mazoezi BOFYA HAPA!

Kutokana na umuhimu mkubwa wa mazoezi , swali linakuja kwako msomaji, je ni kwanini hufanyi mazoezi?

Ø  Je, hauna muda?

Ø  Je, una mambo mengine mengi ya kufanya?

Ø  Je, ni kwamba hauna tabia ya kufanya mazoezi?

Ø  Je, ni kwamba hauna mwamko na mazoezi?

Ø  Je, chakula unachokula hakikuruhu kufanya mazoezi?

Ø  Je, wewe ni mnene kupita kiwango hivyo huwezi fanya zoezi hata moja?

 

Ø  Je, hauna sehemu ya kufanyia mazoezi?

Hizi na sababu nyingine nyingi ni baadhi tu ya fikra za watu wengi na jinsi wanavyoyachukulia mazoezi.

Je , nifanye nini ili nianze kufanya mazoezi?

1.       Anza kwa kuandika malengo yako kabla ya kuanza kufanya mazoezi sababu yataweza kukusaidia kukumbuka kwa nini ulianza na hivyo kukupa mwamko wa kuendelea.

2.       Tafuta nguo za mazoezi (si lazima) kwa lengo la kukufanya uwe free wakati wa kufanya mazoezi kutegemea na nguo unazopendelea, zaweza kuwa za kubana au kutepweta kulingana na aina ya zoezi unalotaka kufanya.

3.       Tafuta kiongeza molari, hapa nikimaanisha uwe na simu au chanzo cha mziki ambayo itakusaidia kipindi chote cha mazoezi kukufanya uendelee na mazoezi. Pia kwenye utumiaji wa simu, unaweza pakua application katika stoo ya google ambazo zitakusaidia katika kuhesabu umbali, hatua na kiwango cha mafuta unachotegemea kuchoma bila kusahau kuwa zinaweza kutunza taarifa za mabadiliko ya mwili yanayoweza kutokea kama vile kupungua uzito kwa muda wote utakaokuwa unaitumia.

Waweza pakua app mojawapo kwa ku-BOFYA HAPA

 

4.       Tafuta mwenza (partner) ambaye naye anapenda mazoezi. Hii itakusaidia kuweza kukumbshwa siku zote muda wa mazoezi ukifika. Vile vile itasaidia kama mnafanya zoezi la kukimbia kuweza kuanzisha nyimbo (chenja) njiani kipindi chote mtakachokuwa mnafanya mazoezi.

Mwisho, hakuna sababu ya msingi sana ya kumfanya mtu mwenye afya njema kutokupenda kufanya mazoezi. Utafiti unaonesha kuwa kwa wiki mtu anatakiwa afanye mazoezi kwa dakika 150 au zaidi, ikimaanisha ni kama kutumia dakika zisizopungua 20 au zaidi kila siku ambazo pia unaweza zigawa katika dakika 10 hvyo kufanya mazoezi mara 2 kwa siku kwa huo muda wa dakika 10 ukihakikisha unayafanya kama inavyotatikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center