Tumbo kuchafuka ghafla safarini(Food poisoning): Sababu, Dalili, Nini kifanyike?

tumbo kuchafuka safarini (food poisoning)

Tumbo kuchafuka wakati wa safari ingekuwa vyema kiasi gani kama ungepata alarm au kengele kabla ya kuchafuka hasa unapokuwa safarini?

Mchafuko wa tumbo au kujisikia kupata haja kubwa ghafla(kuhara) ni hali ya kawaida kwani kitaalamu ni mwili unajaribu kutoa sumu iliyopo mwilini iliyozalishwa na vijidudu kama bakteria.

sababu za tumbo kuchafuka

Mara nyingi visababishi vya tumbo kuchafuka wakati wa safari huwa ni kutokana na vyakula tunavyokula wakati wa safari ambavyo huwa vimeingiliwa na vijidudu aina ya bakteria hasa E.coli, Salmonella, Listeria, Campylobacter na C.botulism
Japo vijidudu kama parasiti na virusi pia huweza kusababisha wakiingia kwenye chakula
.

Vyakula vyenye uwezekano mkubwa wa kufanya upate mchafuko wa tumbo

Nyama za ng'ombe na kuku zisizoiva vizuri

Mboga mboga au salad zinazoliwa zikiwa mbichi au hazikuiva vizuri

Mayai yasiyoiva vizuri

Matunda yasiyooshwa vizuri

Wali uliopikwa na kukaa muda mrefu

Maziwa yasiyochemshwa vizuri

Dalili za Tumbo Kuchafuka

Dalili huweza kuanza kujitokeza ndani ya lisaa limoja hadi siku 28 baada ya kula

Kusikia kichefuchefu

 

Kutapika

 

Tumbo kujaa gesi

 

Tumbo kuuma

 

Homa/Joto kupanda

Kama anatapika hakikisha anakunywa maji kadiri anavyoweza na kunywa mengi pale kichefuchefu kimeisha

Mpe maji asukutue mdomo kama anasikia kichefuchefu ila hatapiki

Kama anatapika sana na kuhara kwa wakati mmoja ni vyema akawahishwa hospitali na kuacha kuendelea na safari

Epuka kumpa vyakula vyenya mafuta na vitamu kwani vinaweza sababisha kutapika zaidi

Hakikisha yafuatayo ili adha ya mchafuko wa tumbo usikukute

Kula chakula kilichoiva vizuri

Uliza chakula kimepikwa muda gani kabla hujala

Osha matunda kwa maji safi kabla hujala

Jiepushe na mbogamboga au salad zisizoiva vizuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center