Fahamu tatizo la ukavu ukeni

 • Tatizo la kuwa na ukavu ukeni hutokea wakati tishu za uke hukosa ute wa kutosha na uke kutokua na afya thabiti.
  Kwa kawaida, kuta za uke hukaa zimehifadhiwa na safu nyembamba ya ute maji.
  Hormoni estrojeni husaidia kudumisha uwepo wa ute maji na kuhakikisha uke wako kuwa na afya.
  Kupungua kwa viwango vya estrojeni hupunguza kiasi cha unyevu katika uke. Na
  kupungua kwa homoni kunaweza kutokea wakati wowote kutokana na sababu
  mbalimbali
 • Inaweza kuchukuliwa kama masihara. Lakini ukosefu wa unyevu wa ukeni unaweza kuwa na athari kubwa kwenye maisha yako katika tendo la ndoa.

Kwa bahati nzuri, matibabu kadhaa hupatikana ili kupunguza ukavu wa uke.
Moja kama tatizo ni la muda mrefu ni vema kuonana na daktari aweze kukupa
matibabu au kukushauri kuhusu matumizi ya estrojeni za uke au matumizi ya vilainishi uke.

Matibabu mbadala ya ukavu ukeni ni kama.
Chembe katika maharagwe ya soya huwa na athari sawa na za estrojeni. Ikiwa unatumia kwa wingi soya kwenye lishe yako, unaweza kupata unafuu wa ukavu wa uke.
Ulaji wa mihogo ni kiungo kingine cha ziada ambacho kimeonyesha kusaidia
ku punguza ukavu lakini ushahidi kutoka kwa utafiti bado haujafanyika.


Pia ulaji wa maparachichi, apples, flaxseeds, na kunywa maji mara kwa mara. Ni njia mbadala yenye afya kwa wale ambao hawapendi soya.


Kupaka Mafuta ya Nazi husaidia kuboresha unyevu nyevu kuliko matumizi ya maji au aina ya gel.


Ukavu wa uke na maumivu yanaweza kumfanya mwanamke asipende tendo la
ndoa, japokua tendo la ndoa pia ndio dawa ya asili ya ukavu wa uke. Wakati mwanamke anaandaliwa kwa tendo la ndoa, mzunguko wa damu kwa tishu zake za uke huongezeka, ambayo inasisimua uzalishaji wa unyevu, na hivyo hupambana na ukavu. Hivyo kuhakikisha kuwa umeandaliwa vizuri kabla ya tendo la ndo
inaweza kusaidia kupunguza ukavu wa uke na kukusaidia kufurahia tendo la ndoa.


 Badilisha sabuni unazotumia Kuosha uke. Gels au sabuni zenye harufu, sabuni, sio
salama kutumia kusafishia uke na bidhaa hizi zinaweza kusababisha maambukizi.
Mara nyingi uke huwa na tabia ya kujisafisha wenyewe mara baada ya kujamiiana
na hedhi, hivyo kuosha zaidi na zaidi kwa kutumia kemikali huingiliana na mfumo
huu. Hivyo ni vema kutumia maji ya vuguvugu yakutosha unapoosha uke.

4 thoughts on “Fahamu tatizo la ukavu ukeni

  1. Mara nyingi inashauriwa kupaka mafuta ya nazi yasio na chemikali sehemu za nje ya uke inaweza kusaidia . Ila kwa kuyapaka ndani ya uke tembelea hospitali kwa daktari husika akupe ruhusa ya kufanya hivyo au akusaidie kwa namna nyingine zaidi. Asante sana kwa swali lako rahma.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show