Je , unafahamu haya kuhusu matumizi ya viagra

Viagra ni dawa iliotengenezwa kwa ajili ya matatizo ya kushindwa kusimamisha uume. Inafanya kazi kwa kupumzisha mishipa yako ya damu na kuongeza mtiririko wa damu kwenye uume wako. Kulingana na utafiti wa hivi karibuni, wawili kati ya wanaume watatu walio na matatizo ya kushindwa kusimamisha uume waliripoti kuwa kuchukua dawa ya Viagra iliboresha uimarishaji wao. Mara nyingi, Viagra inachukua athari ndani ya dakika 30.

Ni kipimo gani cha Viagra ninachohitaji?
Vidonge vya viagra vinakuja vipimo vitatu vya 25mg, 50mg na 100mg gani. Ni kipimo unapaswa kutumia kutibu hali yako inategemea na afya yako ya jumla na jinsi dawa hii inavofanya kazi katika mwili wako.

Nani anaweza kuchukua kiasi cha viagra 50 mg?
50mg ni kipimo cha kawaida cha Viagra. Daktari wako anaweza kupendekeza ikiwa unachukua Viagra kwa mara ya kwanza. Kwa wanaume wengi kipimo hiki kinatosha kutibu tatizo la kushindwa kusimamisha uume na kuboresha uzoefu wao wa tendo la ndoa.

Nani anatakiwa kutumia kipimo cha 100mg?
100mg ni kipimo kikubwa cha Viagra. Usichukue zaidi ya 100mg kwa siku. Vidonge vya viagra vya kiasi cha 100mg vinafaa kwa wanaume ambao hushindwa kusimamisha uume kiasi cha kuuingiza ukeni pale wanapotumia kipimo cha 50mg. Unapaswa kujaribu kipimo cha 50mg kwanza na kuongeza tu mpaka kiasi cha 100mg ikiwa uume bado hausimami. Pia unapaswa kuzungumza na daktari wako kabla ya kubadilisha kipimo chako.

Kipimo cha 25mg ni kwa?
Vidonge vya viagra 25mg ni kipimo cha chini kabisa. Unaweza tumia hichi kipimo ikiwa unachukua aina fulani za dawa. Kwa mfano, madawa ya kudhibiti VVU au dawa za kutibu shinikizo la damu. Kuchukua dawa za shinikizo la damu (ugonjwa wa moyo) na Viagra wakati huo huo huongeza hatari ya madhara kama vile kusababisha viwango vya chini vya shinikizo la damu na kizunguzungu, ndiyo sababu kipimo cha chini cha viagra kinaweza kufaa zaidi.

Je, kipimo cha Viagra ninahitaji kinategemea uzito wangu?
Bila kujali uzito wako, daktari wako anaweza kuagiza vidonge vya Viagra 50mg kwanza.

Je, kipimo cha Viagra ninahitaji kinategemea na umri wangu?
Kuna hali fulani ki umri zinazoweza kuwa na athari kulingana na kipimo cha dawa. Lakini kwa viagra hakuna ushauri kuhusu kipimo ambacho unatakiwa kuchukua kwa miaka fulani.

Je, naweza kuongeza kipimo kama haifanyi kazi?
Ikiwa unaona kwamba kipimo ulicho nacho ni kidogo sana, uulizia ushauri wa daktari kama unapaswa kuongeza. Ikiwa huna hali yoyote ya matibabu na hautumii dawa nyingine yoyote, unaweza kuongeza kipimo chako kutoka 50mg hadi 100mg. Hata hivyo, unapaswa kumwomba daktari wako ushauri kwanza. Ikiwa unaona kipimo ulicho nacho ni kikubwa sana unaweza tumia kiwango cha chini.

Ni mara ngapi ninaweza kuchukua Viagra?
Tafadhali, usichukue Viagra zaidi ya mara moja kwa siku. Ikiwa unafanya tendo la ndoa mara mbili kwa wiki unaweza kupata dawa tofauti kama “Cialis daily”, hii inafaa mahitaji yako kuliko Viagra. Na Cialis inaweza kuchukuliwa hata kila siku. Ina kipimo cha chini na husaidia pia kusimamisha uume .

Ni nini kitakachotokea endapo nitachukua au kutumia sana?
Kama ilivyo na dawa nyingi, ni muhimu sana kuchukua kipimo hasa ambacho umeagizwa. Kuchukua sana Viagra huongeza hatari yako ya madhara. Inaweza kukusababishwa na shinikizo la damu na ugonjwa wa sonono (drepression). Pia huongeza hatari ya kuwa na ‘priapism’, ambayo ni kudumu kwa uume kusimama. Ikiwa umeona kuwa umechukua Viagra zaidi ya vipimo, unapaswa kutembelea idara ya dharura (emergency) lililopo katika eneo lako mara moja.

 

 

3 thoughts on “Je , unafahamu haya kuhusu matumizi ya viagra

  1. Naomba kuuliza kama nimetumia na mtu nilie kubaliana naye amekataa kufanya nami mapenzi je, ita nizuru kama simufanya mapenzi kwa siku hiyo..

  2. Nashukuru sana
    Mimi niseme ninatatizo la kutosimamisha muda mrefu nikipiga goli moja tuu chali hata sichukui muda mrefu
    Na kingine nikikutana na mwenzangu akinikemea tuu mboo husinyaa
    Sasa basi naomba kuuliza naweza kutumia kati ya hizo dawa pasipo na kufanya mapenzi yaani kama tiba au nikitumia pasipo kufanya mapenzi kuna madhara gani naweza kuyapata? Kama hiyo cialis daily
    Ahsante

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show