Sababu 5 za kuchelewa kukosa hedhi.

Unahofu kwa sababu umechelewa kuona siku zako, na unajua wewe si mjamzito? Kuchelewa kuona siku zako au kuzikosa hutokea kwa sababu mbalimbali ukiacha mimba.

Wanawake wengi huona siku zao baada ya siku 28. Ingawa mzunguko wa hedhi kawaida huweza kutumia siku 21 hadi siku 35. Ikiwa hujapata hedhi katika kipindi hiki, zifuatazo huweza kuwa visababishi:

1. Msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo huweza kubadili homoni zako, kubadilisha ratiba yako ya kila siku, na hata kuathiri sehemu ya ubongo wako unaohusika na kumudu hedhi zako.

Ikiwa unadhani una msongo wa mawazo jaribu kupumzika mara kwa mara, jaribu kufanya mazoezi pia. Hali hii itakupa nafuu na kupunguza msongo wa mawazo.
DAKTARI MKONONI

Msongo wa mawazo huweza kusababisha ukaugua au uzito kushuka au kupanda, ambayo zote yanaweza kuathiri mzunguko wako wa hedhi

2. Uzito mdogo au uliokithiri

Uzito kuwa mdogo au kukithiri huweza kuathiri mzunguko wa hedhi

Kuwa na uzito asilimia 10 chini ya uzito unaosemekana kuwa wa kawaida kwa urefu wako unaweza kubadilisha njia ya kawaida ya kupata hedhi.

Kama uzito mdogo wa mwili unaweza kusababisha mabadiliko ya homoni, hivyo hivyo pia inaweza kusababishwa na uzito mkubwa. kuwa na uzito wa kawaida hurudisha hedhi katika hali ya kawaida. kujua kama uzito wako ni sahihi ingia hapa:

http://daktarimkononi.com/2018/03/15/je-uzito-wako-ni-salama-kwa-afya-yako/

3. Vidonge vya uzazi wa mpango

Unaweza kupata mabadiliko katika mzunguko wako wakati unatumia vidonge vya uzazi wa mpango. Vidonge hivi huwa na homoni ya estrogen na progesini, ambayo huzuia mayai yako kutoka. Inaweza kuchukua hadi miezi sita kwa mzunguko wako kurudi katika hali ya kawaida tena baada ya kuacha vidonge hivyo.

Fahamu Zaidi:Β 
 Inaweza kuchukua hadi miezi sita kwa mzunguko wako kurudi katika 
 hali ya kawaida tena baada ya kuacha vidonge hivyo.

4. Magonjwa ya kudumu & ya mda mrefu

Magonjwa ya muda mrefu kama kisukari yanaweza kuathiri mzunguko wako wa hedhi.

Mabadiliko katika sukari katika damu yanauhusiano mkubwa na mabadiliko ya homoni, hivyo kisukari kisichodhibitiwa kinaweza kusababisha hedhi yako kubadilika.

5. Magonjwa ya tezi ya thyroid

Tezi kutokufanya kazi au kufanya kazi sana huathiri mzunguko wa hedhi kwa kiasi kikubwa. Matatizo ya tezi hii huweza kutibiwa kwa dawa na hedhi ikarudi kama kawaida.

 

ELIMIKA ZAIDI

Tembelea link hii kufahamu ni dalili zipi zisizo salama na kukulazimu umuone daktari

http://daktarimkononi.com/2018/03/02/hedhi-viashiria-sita-6-vya-kumuona-daktari/

5 thoughts on “Sababu 5 za kuchelewa kukosa hedhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center