ugonjwa wa zinaa wa pangusa (chancroid ulcers)

Pangusa ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aitwae Haemophilus ducrey. Huu ni ugonjwa unaosababisha vidonda vyenye maumivu makali katika sehemu za siri za mwanamke na mwanaume pia. Vidonda hivi hutoa maji maji ambayo hubeba mambukizi wakati wa ngongo isiyo salama.

Pangusa huambikizwa wakati wa ngono isiyo salama na mtu mwenye maambukizi haya, bakteria huweza kupita kwenye ngozi laini kama ya uke kirahisi bila hata ya kuwepo kwa michubuko.

Wanawake huweza kuhifadhi bakteria hawa kwa muda mrefu bila kuonesha dalili zozote na kuwaambukiza wanaume wengi.

Zaidi, ugonjwa huu huleta vidonda vikubwa sana sehemu za siri na kusababisha kulika kwa sehemu hizo, na kama tiba isipotolewa mapema huweza kumaliza kabisa sehemu za siri.

Dalili za ugonjwa wa pangusa ni zipi?
Dalili zinatofautiana kati ya mwanamke na mwanaume, dalili hizi huanza kutokea kati ya siku 4 mpaka 7 baada ya mambukizi.

Dalili za pangusa kwa mwanaume.
Mwanaume huanza kuona viupele vidogo vyekundu katika sehemu zake za siri ambavyo baada ya siku 1 au 2 hua vidonda. Vidonda hivi hutokea kwenye uume au kwenye ngozi ya kende/korodani. Vidonda hivi vinauma sana na huongezeka ukubwa kadri ya siku.

Dalili za pangusa kwa mwanamke.
Wanawake pia huanza kwa kupata vipele katika sehemu za nje ya uke, sehemu za aja kubwa au katika mapaja. Baada ya muda, vipele hivi hua vidonda ambapo mwanamke hupata maumivu sana wakati wa kukojoa.

Dalili za pangusa kwa wote.

1. vidonda hivi hutoa damu kiurahisi kama vikishikwa au kuguswa.
2. maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa au wakati wa kukojoa.
3. kuvimba na maumivu sehemu za nyonga (mitoki)
4. kutokwa na usaa kwenye vidonda

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa huu:
1. matumizi sahihi ya kondomu wakati wa kujamiiana.
2. kua na mpenzi mmoja mwaminifu

3. kupata tiba mapema pamoja na mwenza wako endapo zitaonekana dalili tajwa
4. usishiriki ngono kabsa kama huwezi kutumia kondomu au kua mwaminifu.

Ugonjwa huu unatibika, mara uonapo dalili twajwa hapo juu, wahi mapema kitio cha afya kilicho karibu nawe kwa ushauri, vipimo na tiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center