Utunzaji wa kitovu cha mtoto mchanga

Kitovu ni kati ya viungo vinavyohitaji uangalifu wa hali ya juu. Mtoto huzaliwa akiwa bado ameungana na kondo la nyuma (placenta).Mara baada ya mtoto kuzaliwa muunganiko huu hutenganishwa kwa kukatwa, hali hii husababisha mtoto kuwa katika hati hati za kupata maambukizi ya magonjwa tofauti endapo eneo lililo katwa ili kutenganisha muunganiko huo wa mtoto na kondo la nyuma (placenta) hauto tunzwa kwa uangalifu mpaka pale sehemu hiyo itakapo kauka na kujifunga vizuri kutengeneza kitovu.

Mambo muhimu ya kuzingatia

Usafi wa mama na mtoto.

Ni vyema kwa mama au mlezi wa mtoto kuzingatia usafi wa mtoto na wa kwake katika kipindi chote cha huduma kwa mtoto, haswa pindi kitovu cha mtoto kisafishwapo. Hali hii huzuia maambukizi mbalimbali ya magonjwa hatarishi kwa mtoto.

Uangalifu

Ikumbukwe kua kitovu cha mtoto mchanga ni sehemu ya mwili ambayo inahitaji uangalifu wa hali ya juu haswa pindi mama anapokua anamsafisha mtoto. Mama au mlezi wa mtoto anatakiwa kuwa mwangalifu asimtoneshe mtoto na kusababisha maumivu katika eneo la kitovu haswa pale ambapo kidonda kinakua hakija kauka vizuri.

Ukavu katika eneo la kitovu

Eneo la kitovu hutakiwa kubaki likiwa kavu muda wote, hii hupunguza uwezekano wa mtoto kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali na pia husaidia katika uponaji wa eneo hilo kwa wakati.
Vilevile uangalifu pindi mtoto anapo ogeshwa, eneo la kitovu hupaswa kusafishwa kwa uangalifu ili maji yasiingie. Ni vyema kama mama au mlezi wa mtoto atatumia kitambaa chenye unyevunyevu anapokua anasafisha eneo hili.

Kumbuka; Usisite kumpeleka mtoto katika kituo cha afya chochote kilichopo karibu endapo kutakuwa na mabadiliko yoyote yasio ya kawaida katika eneo la kitovu cha mtoto.Β Mfano; mabadiliko ya rangi, kitovu kutoa usaha au harufu katika kitovu cha mtoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center