Huduma ya kwanza kwa majeruhi aliye pigwa shoti ya umeme.

.

Ni jambo la dharura!

Mara nyingi hatari za umeme katika mazingira yetu hutokea, na tumekua tukishuhudia watu wakipata madhara mbalimbali kutokana na ajali hizo  ikiwemo ulemavu wa kudumu na hata kupoteza Maisha baada ya ajali hizo.

Leo ningependa tuzungumzie namna ya kusaidia kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliye pigwa na shoti ya umeme.Madhara yanayo tokana na umeme hutegemea hasa kiwango cha mkondo wa umeme unaopita katika chanzo hicho cha umeme  na aina ya umeme, kama inavyo julikana kuna aina mbili za umeme direct current (DC)  na alternate current (AC). Hivyo madhara ya umeme kwa majeruhi hutegemea pande hizo zote mbili. Kama inavyo fahamika mwili wa binadamu ni kipitishio kizuri cha umeme hivyo anapo pata  athari za umeme madhara ya umeme huwa ni kwa kiasi kikubwa na matibabu ya haraka huhitajika na uangalizi wa karibu kwa mgojwa.

Shoti ya umeme kwa mtu huweza kusababisha mtu kuungua na kupata vidonda vya kuungua,pia huweza kuleta alama za shoti kwenye ngozi ama zisiwepo,pia katika baadhi ya matukio mgonjwa anapopata madhara ya umeme na umeme ukapita ndani ya mwili huleta madhara ndani ya mwili kama vile madhara ya moyo kuzima na kushindwa kupiga kwa ghafla ambayo kitaalamu huitwa cardiac arrest, na katika hatua hiyo madhara ya shoti ya umeme ni makubwa.

HATUA ZA KUTOA HUDUMA YA KWANZA.

1.MTENGANISHE MAJERUHI NA CHANZO CHA UMEME

Hii ni hatua ya kwanza kwa muathirika wa ajali ya umeme, INGAWA TUNATOA ANGALIZO HUSIMSHIKE MAJERUHI WA UMEME KAMA BADO HUJAZIMA CHANZO CHA UMEME KWANI UNAJIWEKA KATIKA HATARI YA WEWE PIA KUPIGWA SHOTI YA UMEME PIA.

Tafuta chanzo  na zima umeme  kama ni katika nyumba tafuta sakiti kuu au circuit breaker na uzime kwanza kuzuia mwendelezo wa umeme ,Na kama utashindwa kufikia chanzo cha sakiti basi simama kwenye kitu kikavu kama vile kitabu au gazeti au mbao kavu,tumia mti mkavu  kumtoa majeruhi katika umeme.

Na kama chanzo cha umeme ni kikubwa basi watafute wahusika wa umeme wazime chanzo kikuu cha umeme..

  1. ANGALIA KAMA MAJERUHI ANAPUUA VIZURI.

Baada ya kumsaidia majeruhi kutoka katika chanzo cha umeme zingatia kama mgonjwa anapumua vizuri na kama hapumui vizuri basi msaidie kupumua vizuri kama unafahamu kusaidia kutoa huduma ya kwanza kwa mtu ambaye kapoteza pumzi, na kama huwezi basi mwarakishe mgonjwa hospitali.

3.ANGALIA KAMA KUNA MAJERAHA

Ni vizuri kukagua kama majeruhi anatoka damu na saidia kuzuia damu isiendelee kutoka,kama kuna kidonda msaidie majeruhi kufunika kidonda kwa kitambaa safi na majeruhi afikishwe katika kituo cha afya mapema.

IKUMBUKWE KUWA.

Ajali ya umeme ni dharura ni vizuri kumpeleka majeruhi hospitali hata kama mgonjwa hana dalili yoyote,lakini  endapo utamwona majeruhi ana dalili zifuatazo mpeleke majeruhi hospitali mapema zaidi miongoni mwa dalili hizo ni

  • Majeruhi kaungua sehemu kubwa ya mwili.
  • Majeruhi anachanganyikiwa na kupoteza fahamu.
  • Mgonjwa anashindwa kupumua vizuri.
  • Majeruhi anapata kifafa baada ya ajali.
  • Majeruhi kupata maumivu makali ya misuli.
  • Kubadilika kwa mapigo ya moyo ya mgonjwa na moyo kuzima kwa ghafula.

Tupe sapoti yako kwa kusambaza Makala hii pia kwa wengine wapate kufahamu,usisite kutupa maoni yako na maswali katika kisanduku hapa chini.

2 thoughts on “Huduma ya kwanza kwa majeruhi aliye pigwa shoti ya umeme.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center