Dawa muhimu kuwa nazo nyumbani.

Ni kawaida kwa binadamu kupatwa na maumivu au maradhi madogo madogo mara kwa mara hasa watoto wadogo. Dalili nyingi huanza wakati tusiotarajia na pengine tunashindwa kuapata msaada wa haraka. Haya baadhi ya mapendekezo ya dawa ambazo yafaa kuwa nazo nyumbani zikusaidie wakati wa shida au dharura.聽聽

Zingatia!!!

  • Kabla ya kutumia dawa, daima usome lebo ya pakiti na kipeperushi ndani ya pakiti. Hii ni kwa ajili ya maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa na juu ya nani asiyepaswa kutumia dawa hii pia kwa orodha ya madhara yanayoweza kusababishwa na dawa(side effects).

  • Weka dawa mbali na watoto.
  • Wajawazito waepuke sana kutumia dawa bila maelekezo ya daktari kwani baadhi ya dawa humdhuru mtoto tumboni.

Paracetamol (panadol)

Paracetamol hutuliza maumivu na homa. Inapatikana kwa njia ya vidonge kwa watu wazima na majimaji kwa watoto wadogo. Ikiwa una watoto wadogo, paracetamol yaweza kuwa ni dawa muhimu kuliko zote kwako. Paracetamol ni salama kwa kiwango cha kawaida lakini ni hatari unapokunywa nyingi mno (overdose).

Dawa za kutuliza maumivu za Anti-inflammatory

Hizi ni dawa za kutuliza maumivu ambazo pia hupunguza kuvimba. Husaidia kwa maumivu ya misuli na vidonda, maumivu ya hedhi na pia hushusha homa. Kunywa dawa hizi pamoja na chakula kuepusha vidonda vya tumbo. m.f. Ibuprofen, Aspirin, Naproxen

Antihistamini.

Hizi hupunguza dalili zote za aleji -m.f. Aleji za ngozi(urticaria), kuwahswa, kupiga chafya, kutokwa na machozi mno, mafua makali, n.k. Inaweza pia kutumika kutuliza maumivu na uvimbe kwa aliyengatwa na nyuki, dondora, na wadudu mbalimbali.
Antihistamini zingine zinaweza kusababisha usingizi m.f. chlorphenamine(Piriton庐), diphenhydramine. Hizi unashauriwa kutumia zaidi usiku. Na ambazo hazileti sana usingizi - m.f. loratadine na cetirizine zinafaa kutumika mchana.
Antihistamine pia hupatikana kama cream, ambayo unaweza kupaka sehemu uliyong鈥檃twa.

Dawa za kuingulia.

Hizi hutuliza asidi tumboni hivyo huondoa kiungulia. m.f. sodium bicarbonate, magnesium trisilicate, aluminium/magnesium hydroxide. Dawa zenye nguvu zaidi ni pantocid, ranitidine na esomeprazole.

Krimu ya Hydrocortisone

Krimu ya Hydrocortisone ni dawa ya steroidi. Na hizi hupunguza kuvimba mwili, ugonjwa wa ngozi, kung鈥檃twa na wadudu na eczema. Usipake dawa hii kwenye uso isipokuwa kwa maelekezo ya daktari.

Dawa ya antiseptic

Hii hutumika kwa ajili ya vidonda vidogo, michubuko na kuumwa na wadudu. Husaidia kuua bacteria na hivyo kidonda kupona mapema zaidi. m.f. hydrogen peroxide, spirit, iodine, polyhexanide, n.k.

Dawa za kuzuia kuharisha.

Kuharisha huisha kwenyewe mara nyingi lakini inapozidi waweza kutumia dawa zifuatazo Loperamide(Imodium), Pepto-Bismol, Kaopectate, n.k.

Dawa hizi ni zaidi kwa ajili kutuliza maumivu na kutuliza dalili za ugonjwa. Muone daktari kwa ajili ya kupata tiba kamili hasa ukijikuta unahitaji kutumia dawa hizi mara kwa mara. Dalili huweza kuwa ishara ya ugonjwa mkubwa zaidi unaendelea kushamiri mwilini mwako.

Watu wenye magonjwa sugu kama asthma, kisukari, shinikizo la damu na mengineyo wahakikishe wanakuwa na dawa za ziada mara zote, usisubiri ziishe kabisa ndipo uende hospitali.聽

Je! kuna dawa muhimu unafikiri imesahaulika? Tafadhali聽 comment hapo chini kuwasaidia wengine waongeze dawa hiyo katika orodha yao.

4 thoughts on “Dawa muhimu kuwa nazo nyumbani.

  1. This is very nice article. Would just like to recommend if you could mention some examples of the medicines you’ve stated above. Thank you

  2. Asante kwa elimu na tarifaa zenye manufaa ulizotupatia.Katika hilo pia napendekeza na hivyo kutoa changamoto juu ya elimu tolewa. Suala la kukaa na dawa nyumbani limekuwa na changamoto sana hususani suala zima la ufahamu juu ya utunzaji na mazigira sahihi ya kuweka dawa hizo, tarehe ya kuisha muda wa matumizi wa dawa, utumiaji holela wa dawa zilizoifadhiwa nyumbani, kiwago cha dawa kinachoitajika (dose), wakati mwingine tiba binafsi (self medication) imesababisha matumizi ya dawa yaso na tija alikadhalika kudhofisha mwili ( irrational use of drug). Yote haya ni miongoni mwa changamoto. Hata ivyo suala zima katika elimu hii inatakiwa lisisitizwe sambamba na kuhakikisha matumizi ya dawa tajwa (otc’s) kuwa bado yanaitaji ushauri au elimu ya kutosha kutoka kwa wataalumu wa dawa kwenda kwa watumiaji ili kuhakikisha panakuna na tiba binafsi yenye matokeo chanya (rational self medication)

  3. Elimu zaidi inahitajika juu ya matumizi sahihi ya dawa kwa sababu jamii kubwa haiwezi kusoma maelezo ya kwny kipeperushi kutokana na lugha iliyotumika.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center