Umuhimu wa kunywa maji mengi mwillini.

Maji ni uhai kwani miili yetu huundwa na asilimia 70 ya maji, hivyo ni muhimu kunywa maji ya kutosha ili kuufanya mwili kufanya kazi vyema. Ikitokea mwili haupati maji ya kutosha madhara mbalimbali ya muda mfupi na muda mrefu huweza kutokea.

·         Kupunguza uzito    Kunywa maji mengi kunasaidia kupunguza uzito, kwani maji hayana mafuta, kalori wala sukari. Ukiliganisha na vinywaji kama soda vyenye sukari na kalori nyingi ambavyo hupelekea kuongezeka uzito.

·       Huboresha metaboli na Nishati ya mwili                            Metaboli ni mchakato ambao mwilli hutumia kutengeneza nguvu na kujijenga kutokana na  vyakula (wanga, protini na mafuta). Hivyo basi, unywaji wa maji huwezesha mchakato huu kwenda vyema na kuufanya mwili kuwa na afya njema. Mwili unapopungikiwa maji, hukufanya ujisikie mchovu, hivyo kwa kunywa maji ya kutosha daima utakuwa mwenye nguvu

·       Tiba ya kichwa         Kuumwa kichwa husababishwa na vitu vingi ikiwemo kupungukiwa na maji mwilini hivyo basi Kunywa maji ya kutosha kutasaidia kupooza maumivu ya kichwa.

·         Ngozi nyororo:               Unywaji maji ya kutosha kila siku husaidia kusafisha ngozi yako na kuifanya ionekane nyororo kwani maji huongeza na kurahisisha mzunguko mzuri wa damu katika ngozi na hili hupelekea kuondoa sumu mbalimbali katika ngozi na kuiacha ngozi yako katika hali nzuri kiafya.

·       Huzuia kutengenezeka kwa mawe kwenye figo:

Unywaji wa maji huzimua asidi inayosababisha mawe kwenye figo ambayo hupatikana tumboni. Kumywa maji ya kutosha husaidia utendaji kazi wa figo.

 

·       Usafishaji wa mwili:

Maji husaidia kuondoa sumu mwilini kwa kutoa uchafu wote kwa njia ya mkojo na haja kubwa. Pia Unapokunywa maji kabla ya kula chochote asubuhi utauwezesha mwili wako kujenga misuli na kuzalisha seli mpya za damu.

 

·       Saratarani:

Utajiepusha na saratani ya tumbo kwa kunywa maji, kwani maji husaidia suala la usagaji wa chakula tumboni, pia unapunguza uwezekano wa kupata kupata saratani  kwa saratani ya kibofu cha mkojo.

Privacy Preference Center