Nitumie kinywaji/chakula gani ninapotaka kumeza dawa?

Unajua kuhusu muingiliano wa dawa?

Aina ya vyakula, vinywaji, pombe, kahawa, na hata sigara huweza kuleta muingiliano vikitumika pamoja na Dawa. Kwa ujumla, Maji ndio kimiminika kinachotakiwa na ni kizuri kwa ajili ya kunywea dawa.

Japokua maji hufahamika kama kimiminika chenye ubora kwa kunywea dawa, maji hayo hayo huweza kushindwa kutumika kwa ajili ya dawa. Mfano: dawa zenye kemikali aina ya Aspirini huweza kusababisha maumivu ya tumbo na hivo kutumia maziwa kunywea dawa hizi huweza kusaidia kuzuia matatizo haya. Pia Dawa nyingine kwa mfano dawa ya fangasi iitwayo ‘Griseofulvin’ hufanya kazi vizuri mwilini pindi inapomezwa pamoja na chakula, hasa hasa vyakula vya mafuta.

Inakupasa uwasiliane na mganga/daktari wako au mfamasia wako kwa ajili ya ushauri zaidi.

Mifano mingine ambayo huweza kuleta madhara makubwa pindi dawa hizi zinaponywewa na kimiminika au chakula cha aina flani ni kama:

 • Matumizi ya pombe pamoja na dawa kwa ajili ya aleji (antihistamines) huweza kusababisha uchovu wa hali ya juu.
 • Matumizi ya pombe pamoja na dawa zenye kemikali aina ya aspirini au acetaminophen (al-maarufu kama Panadol/Paracetamol) kwa ajili ya maumivu huweza kusababisha kuharibika kwa ini.
 • Matumizi ya vinywaji vyenye kemikali aina ya kafeini ambayo hupatikana hasa kwenye kahawa au soda (hasa Coca-Cola) pamoja na dawa za pumu za kuvuta (inhalers) kwa ajili ya pumu au magonjwa mengine yanayoleta usumbufu katika njia ya hewa au kupumua huweza kusababisha dawa hiyo kutokufanya kazi yake vizuri.
 • Matumizi ya vyakula vya aina flani pamoja na matumizi ya dawa za kutibu presha huweza kupunguza mmeng’enyo wa dawa hiyo katika mwili hivyo kushindwa kufanya kazi yake.

Mgonjwa hushauriwa kuulizia zaidi juu ya matumizi ya dawa alizopatiwa na jinsi ya kuzimeza na pia kupewa ushauri zaidi juu ya matatizo au madhara ambayo anaweza kuyapata kwa kutumia dawa hizo. Muuguzi pamoja na waganga wanapaswa kua makini katika kutoa maelezo juu ya dawa wanazowaandikia wagonjwa.

2 thoughts on “Nitumie kinywaji/chakula gani ninapotaka kumeza dawa?

 1. Asante kwa Elimu nzuri kuhusiana na muingiliano wa dawa na vyakula na kwa kuwa leo ni siku ya Wafamasia duniani tungependa kuwashauri wahudumu wote wa afya pamoja na wagonjwa kwamba ni vyema wakapata ushauri kutoka kwa experts wa madawa(pharmacist)
  ili kuepusha matatizo ama vifo vitokanavyo na matumizi ya dawa yasiyo sahihi.
  Asante.

  1. Habari yako Mwamakula. Ahsante kwa kuendelea kujumuika nasi katika kuelimisha jamii.
   Ni kweli yatupasa kuafuata ushauri wa wafamasia juu ya madawa kwa ajili ya matumizi sahihi zaidi ya dawa. Tuendeleee kutoa elimu kwa jamii juu ya watu sahihi wa kuulizwa pindi wakiwa na swali lolote juu ya dawa.
   Endelea kufurahia nasi kuelimisha watu kupitia daktarimkononi😊😊 ahsante

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center