Bima ya Afya (NHIF)

UJUE MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

NHIF ilianzishwa ili kusimamia upatikanaji wa huduma za matibabu kwaΒ 

 • Watumishi wa serikali
 • Umma
 • Binafsi
 • Wanafunzi
 • Na makundi mbalimbali ya watu
Lengo likiwa ni kupata huduma za matibabu kupitia vituo vya serikali, madhehebu ya dini, binafsi, na maduka ya dawa ambayo yamesajiliwa na mfuko.

MAFAO

Tuna kitita kipana cha mafao kwa wanachama

WATEGEMEZI

Mwanachama ana nafasi ya kusajili wategemzi wake

VITUO

Tuna mtandao mpana wa vituo zaidi ya 6,500 nchini

KADI

Kadi hutumiwa katika vituo vyote vya afya vilivyosajiliwa

Toto Afya kadi
Huduma mpya na bora

Katika kutanua wigo wa uanachama, NHIF sasa inasajili watoto katika huduma zake ijulikanayo kama NHIF toto afya kadi kwa ajili ya watoto wenye umri chini ya miaka 18.

MAFAO
2500
VITUO
VIPIMO

Tupo kwa ajili yako.

Huduma bora za matibabu ni haki yako na ni dhamana yetu!

Maswali na majibu

Kuna mfuko wa bima ya afya kwa ajili ya watumishi wa madhehebu ya dini. Ambapo masheikh, maimamu, maaskofu, mapadre, masista na makundi mengine yanaweza kujiunga.

NHIF ina mfuko kwa ajili ya vifaa tiba, ujenzi, ukarabati wa majengo, na dawa kwa azma ya kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya na Tanzania kwa ujumla

Wakulima wanaweza kuungana kwa pamoja katika vyama vya ushirika ambapo watapata nafasi ya kujiunga na bima ya afya kwa utaratibu wa ushirika afya.

ushuhuda

NHIF imenisaidia sana kama mwanafunzi katika kipindi changu cha masomo ikiwa imenirahisishia matibabu.
Joseph Paul
Mwanafunzi
Mfuko wa bima ya afya ya taifa (NHIF) umekua msaada mkubwa katika matibabu na vipimo. Nawashukuru na muendelee na kazi nzuri.
Joseph Mwalongo
Mwanafunzi

15 thoughts on “Bima ya Afya (NHIF)

 1. Shukran sana Daktari Mkononi kwa kutuelimisha tena na tena kuhusu maswala ya afya hasa kuhusu swala la bima ya Afya.
  Swali langu ni Je naweza lipia bima zaidi ya mwaka mmoja mfano miaka mitano?

 2. Hivi majuzi tulisikia naibu waziri wa Afya akizungumzia kuhusu bima ya Afya kuju na mkakati wa Kama vifurushi au bundle Je utawafaidisha vipi watu wa kipato cha chini kama machinga na makondakta pamoja na mama ntilie?

 3. Yani mmerahisisha sana upatikanaji wa afyaaa mavyuoni………. shukrani sana…
  Toto bima bado haifahamiki mtaani, ni mbinu nzuri sana ya kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitanoo…. hongereni kwa kazi nzuriii

 4. Asanteni NHIF kwa huduma yenu. Je, kwa wale wenye kipato cha chini wasioweza kulipia gharama za huduma ya afya na wanaohitaji sana kuhudumiwa mna mikakati gani ya kuwafikia na hao? Hata kama sio endelevu lakini pale wanapohitaji huduma na hawawezi kulipia

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center