huduma ya kwanza kwa mtu aliye bakwa

1. Hakikisha Usalama wa muathirika

Muweke muathirika katika mazingira salama na pia jaribu kumuweka eneo lenye uangalizi. Unaweza waita polisi ikiwa bado kuna ishara za hatari kutoka kwa mshambulizi.

2. Toa Msaada

uhakikishe muathirika asije achwa peke yake. Fuata kwa kutafuta kituo cha afya chochote kilichopo maeneo ya karibu.

3. Asijisafishe Kabla ya Kupata Uangalizi wa kitabibu.

Ili kuzuia ushahidi, muathirika hapaswi kuoga, au kubadilisha nguo mpaka apate uchunguzi na matibabu. Usifute chochote kwenye eneo la tukio hilo.

4.Tafuta haraka Matibabu kutoka kwa Daktari

daktari huweza kukusanya nywele, shahawa, nyuzi za nguo, na ushahidi mwingine wa utambulisho wa mshambulizi.Hata kama aliyeathiriwa haitaji  kutoa ripoti ya shambulio hilo, bado ni muhimu kukusanya na kuhifadhi habari ili ziweze kupatikana katika tarehe ya baadaye, ikiwa ni lazima.

5. ufuatiliaji

 Daktari hutibu majeraha  yaliyo tokana na ubakaji. Waathirika wanapaswa kutibiwa au kuangaliwa kama wanadalili yoyote ya magonjwa ya zinaa (STDs) na pia hupewa dawa za uzazi wa mpango za dharura. Ni muhimu kupokea dawa za uzazi wa mpango na matibabu dhidi ya magonjwa ta zinaa ndani na masaa 72 ya mwanzo kwa ufanisi mkubwa. Pia muathirika anaweza pata msaada wa washauri wa afya ya akili ambao wanaweza kusaidia yule aliyeathirika na shida ya ubakaji kutokua na athari kubwa ya kisaokolojia. Ni vyema kufahamu kua utoaji msaada wa kiafya na wa kisaikolojia kwa waathirika wa ubakaji ni muhimu, kwa sababu uponyaji wao huitaji miaka mingi.

3 thoughts on “huduma ya kwanza kwa mtu aliye bakwa

  1. Asante sana kutujuza haya,nadhani jamii inapaswa kuhakikisha muathiriwa wa tukio la kubakwa anawaishwa hospital,Maana hii ni changamoto hasa kama tendo limetokea nyumbani miongoni mwa ndugu,utasikia tulikaa kwanza kikao cha familia,hapo ushaidi wa kitabibu unapotea,na siku za kuanza PEP zinapita.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center