Ugonjwa wa kukaza kwa misuli ya Uke(Vaginismus)

Ugonjwa wa kukaza kwa misuli ya Uke (Vaginismus)

Wanawake wengi hupatwa tatizo la misuli ya uke hukaza yenyewe wakati kitu chochote kikijaribu kupenya ukeni. Hii kitaalamu hujulikana kama "vaginismus", misuli ikikaza inaweza kuzuia kujamiana au huweza kufanya tendo la ndoa kuwa na maumivu sana.

Hii huweza tokea :

  • Pale mpenzi wako akijaribu kupenya ukeni.
  •  Wakati mwanamke akijaribu kuingiza tamponi ya hedhi.
  • Au mwanamke akiguswa au kugusa karibu na eneo la Uke

Kukaza kwa misuli ya uke haiusiani na muamko wa kimapenzi katika kufika kileleni bali huzuia uume kupenya ukeni.

Uchunguzi wa nyonga huonyesha hakuna sababu halisi ya misuli hiyo kukaza, pia hakuna tofauti ya kimaumbile inayochangia hali hiyo.

Kukaza kwa misuli ya uke ipo katika aina mbili

Vaginismus ya awali (primary vaginismus): Hii ni pale ambayo hakujawahi kuwa na uwezekano wowote wa kupenya ukeni.

Vaginismus aina ya pili (secondary vaginismus):  hii ni ile ambayo Uingiaji ukeni ulishawahi tokea  mara moja lakini haikuwezekana tena  kwa mara nyingine na nikutokana na sababu kama vile upasuaji, majeraha au mionzi. 

Sababu za Misuli ya Uke Kukaza.

Wataalamu hawajui nini chanzo cha misuli ya uke kukaza bali wamehusisha na hofu na wasiwasi kuhusu tendo la ndoa , lakini haijulikani kipi huanza kati ya kukaza kwa misuli ya uke au hofu na wasiwasi.

Wanawake wengine hupatwa na tatizo hilo katika hali zote na kwa kitu chochote. Wengine wana hali hiyo kwa mpenzi mmoja au wakati wa kujamiana na sio kwa kuvaa tamponi au wakati wa matibabu.

Matatizo mengine kama maambukizi ya magonjwa yanaweza pia kusababisha maumivu ya wakati wa tendo la ndoa, kwa hiyo ni muhimu kumuona daktari kutambua sababu kuu ya maumivu wakati wa tendo la ndoa.

MATIBABU

Wanawake wenye matatizo ya misuli kukaza wanaweza fanya mazoezi wakiwa peke yao ili kujifunza kudhibiti ukazaji wa misuli na kuzoea kupumzisha misuli karibu na uke.

Njia hii husaidia kurahisissha kupenya katika uke bila maumivu

Kwanza, fanya mazoezi ya kegeli https://daktarimkononi.com/2018/07/25/fahamu-juu-ya-mazoezi-ya-kuimarisha-misuli-ya-nyonga-zako-kegel-excercises/

Unaweza fanya Kegels 20 kwa wakati mmoja , pia unawea fanya mara nyingi utakavyo kwa siku moja.

Baada ya siku chache, ingiza kidole kimoja mpaka nusu kidole ndani ya uke wakati wa kufanya mazoezi. ni vizuri kutumia vilainishi au kufanya zoezi hilo bafuni na kutumia maji kama kilainishi.

Anza kwa kuweka kidole kimoja mpaka vitatu.  Utasikia misuli ya uke ikibana karibu na kidole chako na unaweza toa kidole kila ukiwa hauko na wakati mzuri na mazoezi.

Wanawake ambao kukaza kwa uke kunahusiana na hofu au wasiwasi wa tendo la ndoa tiba ya shirikishi husaidia. 

1 thought on “Ugonjwa wa kukaza kwa misuli ya Uke(Vaginismus)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center