fahamu kuhusu magonjwa ya zinaa.(part 1)

dalili muhimu.....

Neno gonjwa ya zinaa (STD)  hutokana na usambazaji wa maradhi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya ngono. Unaweza pata maambukizi kupitia ngono isizo salama au katika kufanya mapenzi kinyume na maumbile, na mtu aliye kwisha athirika na magonjwa ya zinaa.

 

Ngono isio salama sio njia pekee ya kusambaza magonjwa ya zinaa. Maambukizi yanaweza pia kusambazwa kupitia sindano za kugawana na viwembe au kifaa chochote chenye ncha kali kisicho salama na pia hata kwa kunyonyesha.

 

 

Dalili za magonjwa ya zinaa kwa wanaume.

 • maumivu wakati wa tendo la ndoa au kukojoa.
 • vidonda karibu na uume.
 • vipele maeneo ya uume,karibu na shimo la haja kubwa, kwenye mapaja, au vidonda kwenye kinywa
 • kutokwa na damu katika uume
 • maumivu makali au kuvimba sehemu za siri.

 

Dalili za magonjwa ya zinaa kwa wanawake.

Dalili kwa wanawake ni pamoja na;

 • maumivu wakati wa tendo au kukojoa.
 • vidonda karibu na uke.
 • vipele maeneo ya uke,karibu na shimo la haja kubwa, kwenye mapaja, au vidonda kwenye kinywa
 • kutokwa na damu ukeni.
 • maumivu makali au kuvimba sehemu za siri.
 • Kuwashwa sehemu za siri.

Fahamu kuwa dalili zinaweza kutofautiana, kulingana na aina ya gonjwa la zinaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center