FAHAMU JUU YA DALILI ZA AWALI ZA MAAMBUKIZI YA VVU!.

VIRUSI VYA UKIMWI!

Kwa kifupi huitwa VVU, ni vimelea ambavyo hushambulia chembechembe za mwili zinazohusika na ulinzi wa mwili dhidi ya magonjwa. VVU hushambulia chembechembe za CD4 na CD8 ambazo hupelekea kupungua kwa chembechembe hizi na kusababisha magonjwa nyemelezi kushambulia mwili.

Katika mwili wa binadamu idadi ya CD4 huwa ni kuanzia 500 mpaka 1400 ya ujazo katika milimita.

Kwa makadirio ya watu 7 mpaka 8 kati ya 10 wanaopata maambukizi ya awali huonesha dalili baada ya wiki 2 mpaka 4 baada ya kuambukizwa VVU.

Dalili hizo ni kama;

 • Homa,
 • Kupata ukurutu katika ngozi,
 • Maumivu ya misuli na viungo,
 • Mwili kuchoka na kuishiwa nguvu, pia
 • Kuvimba kwa koo na matezi ya shingo.

Dalili hizi hupona baada ya wiki 1 mpaka 2 na mara chache huchukua wiki zisizopungua 10. Njia pekee ya kuweza kujua kama dalili hizi zinahusiana na maambukizi ya VVU ni kupima uwepo wa VVU katika umajimaji (serum) ya damu.

Kwa kawaida si dalili zote za awali huisha, dalili ya kuvimba kwa matezi huendelea kuwepo ila huwa ni vigumu kwa mgonjwa kugundua mpaka afanyiwe uchunguzi na daktari. Pia katika maambukizi bila dalili kiwango cha CD4 kinaendelea kushuka kwa kasi kubwa, makadirio ya chembe 50-150 kwa mwaka hufa.

Baada ya miaka 7 mpaka 10 ya kupata maambukizi ya awali na kuishi bila dalili, kinga ya mwili itokanayo na seli huaribiwa. Hii husababisha hali zifuatazo katika mwili wa binadamu;

 • Kupungua kwa uzito, zaidi ya 10% ya uzito bila sababu,
 • Homa,
 • Kuharisha,
 • Fangasi mdomoni au ukeni,
 •  Kupata utando mweupe kinywani.

UKIMWI hutafsiriwa kutokana na uwepo wa magonjwa nyemelezi na uvimbe kulingana na kupungua kwa kiwango cha CD4 kuliko kithiri. UKIMWI hutokea pindi CD4 zimepungua chini ya chembe 200 kwa ujazo.

Baadhi ya magonjwa nyemelezi ni yale yanayoambukizwa na vimelea vya magonjwa kama;

 • Virusi vingine mf. mkanda wa jeshi.
 • Fangasi mf. fangasi za koo.
 • Bakteria mf. watokanao na ndege.

Haya magonjwa nyemelezi pia huambatana na uvimbe wa matezi ya limfu.

Kwa kawaida kuwa na Virusi vya Ukimwi haimaanishi una UKIMWI.  Kama ilivyoelezwa hapo awali, UKIMWI hutokea pale ambapo kinga ya mwili imepungua chini ya chembe 200 kwa ujazo.

Umuhimu wa upimaji na ugunduzi wa VVU mapema!

 1. Husaidia matibabu ya mapema na kurudisha kinga ya mwili katika hali yake ya kawaida.
 2. Husaidia kupunguza uwezekano wa maambukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
 3. Husaidia katika utoaji wa elimu juu ya njia hatarishi zinazoweza sababisha maambukizi ya VVU.

Kwa ufahamu zaidi juu ya VVU/UKIMWI

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center