Kupungua kwa uzito kwa watoto (sababu zake kuu, dalili ambatanishi)

Utangulizi

Kupungua uzito kwa watoto si jambo jema na ni kiashiria kuwa mzazi au mlezi anabidi ampeleke mtoto kituo cha afya mapema isipokuwa pale mtoto akiwa ameshauriwa apunguze uzito kwa uangalizi wa daktari kama hapo mwanzo alikuwa na uzito uliopita kiasi

Sababu kuu za kupungua kwa uzito

Lishe duni

Utoto ni kipindi cha maisha ambapo mwili unakua na huhitaji virutubisho kwa wingi ili kusaidia ukuaji huu, hivyo basi kama vyakula mf. Wanga, protini, matunda na kadhalika vitakuwa ni vya kusuasua hata afya ya mtoto na ukuaji wake kwa ujumla unaweza kuyumba na hata kupelekea mtoto kupungua uzito

Maambukizi

  • Kuna magonjwa yanayosababisha kupungua kwa uzito kwa watoto kama moja ya dalili zake, hivyo ni vyema mzazi/mlezi akajifunza kutambua dalili hizi ambazo zinaweza kuambatana na kupungua kwa uzito na kuwahi hospitalini
  • Dalili ambatanishi ni kama homa, kutapika na kuharisha, kikohozi, maumivu ya sikio, koo au kifua, kupungua kwa kiasi cha mkojo na hata kushindwa kulala

Magonjwa ya kinywa

  • Kama mwanao ana vidonda kwenye kinywa na anakataa kula au kunywa kitu chochote ni dhahiri kwa muda anaweza kupungua uzito kutokana na kula kidogo
  • Hivyo ni vyema ukamwahisha mtoto hospitalini akafanyiwe uchunguzi wa kinywa na kupewa matibabu stahiki ili arejee katika hali yake ya kawaida ya kula kama mtoto mwenye afya njema

Magonjwa ya mfumo wa chakula

  • Matatizo yanayopatikana kwenye mfumo wa chakula kama vidonda vya tumbo, magonjwa ya utumbo mkubwa au mdogo, maambukizi ya wadudu kama amoeba, saratani na mengineyo zote zinaweza kuambatana na kupungua kwa uzito kwa watoto
  • Magonjwa haya yanaweza kuambatana na dalili zingine kama; maumivu ya tumbo, kubadilika kwa tabia ya choo kama kuwa kuharisha, kutokwa kwa damu kwenye choo au hata kupata maumivu wakati wa kujisaidia

Matatizo ya homoni mwiilini

Homoni inayohusika sanasana ni ile ya thyroid ambapo mtoto pamoja na kupungua uzito anaweza kuwa na kama uvimbe kwenye sehemu za shingo, macho kutoka kwa nje, mapigo ya moyo kwenda haraka na kadhalika

Mwisho

โ€ข Kupungua kwa uzito iwe ghafla au kwa kiasi kikubwa ni dalili hatari sana katika ukuaji wa mtoto hivyo ni vyema mtoto akawahishwa hospitalini haraka iwezekanavyo. โ€ข Lakini pia, kulingana na dalili zinazoambatana na kupungua kwa uzito daktari atajua ni matibabu gani yanamfaa mtoto ili arudi katika hali yake ya kawaida

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center