MTOTO WA JICHO (CATARACT)

Mtoto wa jicho, kitaalamu ikijulikana kama Cataract ni ukungu unaojitokeza katika lenzi ya jicho unaosababisha upofu.

Hili ni tatizo linaloongoza kusababisha upofu duniani inakadiriwa kama 50% ya upofu wote duniani.

AINA ZA MTOTO WA JICHO

 1. KUZALIWA NA MTOTO WA JICHO (Congenital/Inborn)

Aina hii ya mtoto wa jicho hutokea endapo ukuaji wa lenzi ya jicho ilipata misukosuko kipindi cha kutengenezewa kwake wakati mtoto akiwa kwenye mfuko wa uzazi na inapelekea mtoto anazaliwa akiwa na mtoto wa jicho.

 1. KUPATA MTOTO WA JICHO (Acquired)

Aina hii ya mtoto wa jicho mtu huipata maishani kwa sababu mbali mbali.

a) Mtoto wa jicho sababu ya uzee (Senile cataract)

Kadiri mtu anavyozidi kuzeeka ndivyo uwezo wa kuona hupungua sababu mojawapo ni ukungu wa lenzi (mtoto wa jicho)

b) Mtoto wa jicho sababu ya kuumia (traumatic cataract)

c) Mtoto wa jicho sababu ya magonjwa mengine ya macho (complicated cataract)

d) Mtoto wa jicho sababu ya mionzi (radiational cataract)

Mionzi ya aina zote yanaweza kuleta mtoto wa jicho (mionzi kama infra-red, ultraviolet). Katika maisha yetu hata mionzi itokanayo na mwanga wa jua huweza kuleta mtoto wa jicho.

e) Mtoto wa jicho sababu ya sumu/madawa (toxic cataract)

f) Mtoto wa jicho itokanayo na matatizo ya mifupa, magonjwa ya Ngozi na magonjwa mengine ya kurithi.

DALILI ZA MTOTO WA JICHO

 • Kuona ukungu, kama moshi moshi au mawingu pasipokua na maumivu
 • kupungua kwa nuru ya kuweza kuona (kitaalamu inaitwa Glare)
 • Kuona picha nyingi ukilenga kuangalia picha moja (kitaalamu inaitwa polyopia diplopia)

 • Inapofikia hatua mtoto wa jicho kukomaa mtu hushindwa kuona kabisa.

MATIBABU YA MTOTO WA JICHO.

 1. Kudhibiti kisababishi cha mtoto wa jicho.

Kudhibiti kisukari

Kuacha kutumia madawa yasababishayo mtoto wa jicho

Kutumia hatua za kuimarisha uonaji kama miwani meusi

2. UPASUAJI– kutolewa lenzi ya jicho na kuwekewa lenzi mpya itakayokuwezesha kuona vizuri.

Je ni watu gani wanaweza kupata mtoto wa jicho?

 1. Wenye umri mkubwa.
 2. Wanaovuta sigara
 3. Wanaokunywa pombe
 4. Wasiokula mlo wenye virutubisho unaofaa kiafya (balanced diet)
 5. Wenye kisukari

2 thoughts on “MTOTO WA JICHO (CATARACT)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show