FAHAMU KUHUSU MAAMBUKIZI YA NJIA YA UPUMUAJI (RESPIRATORY TRACT INFECTIONS).

Maambukizi ya njia ya UPUMUAJI huathiri zaidi njia ya hewa ya kinywa na mapafu. Maambukizi haya huisha ndani ya wiki moja au mbili na pia yanaweza kupona bila kutumia dawa wala kumuona daktari.

 • Kupiga chafya sana
 • Kukohoa kwa kubanja
 • Mafua maji yanayo mwagika
 • Maumivu ya kichwa
 • Maumivu ya misuli
 • Kukosa pumzi,
 • Homa na mwili kuuma
 • Matibabu ya maambukizi ya njia ya pumu  yanaregemeana na chanzo. Kama chanzo ni kirusi, yaani kwasababu ya baridi, inaweza kupona yenyewe baada ya wiki kadhaa na dawa zinaweza zisisaidie. Kama ni cha bacteria mfano pneumonia, unabudi kumuona daktari akupatie sawa.
 • Kwa kawaida unaweza ukajitibu  nyumbani kwa; kunywa maji mengj, kupumzika vizuri, kunywa maji ya moto ya ndimu ama asali hii inafaa sana kwa watoto, kugugulia maji ya moto ya chumvi kwa matatizo ya koo, hii haishauriwi kwa watoto. Kuvuta mvuke wa maji ya moto, hii ni kwa ajili ya watu wazima tu, lala ukiwa umeinua kichwa juu ya mito ili kurahisisha upumuaji.
 • Unaweza ukatumia dawa kwa ajili ya kushusha homa pia kutuliza maumivu ya koo kichwa na misuli ya mwili. Dawa zinazoshauriwa ni kama paracetamol, ibuprofen na hata spray za puani kutuliza dalili zake. Sio kila dawa ni sahihi kwa watoto na wajawazito hivyo watumie dawa wanazoshauriwa na daktari wao
ENDAPO;
 • Dalili zimezidi kuwa dhohofu
 • Ukikohoa damu au kutoa makamasi yenye damu
 • Kukohoa zaidi ya wiki 3
 • Una ujauzito
 • Una miaka zaidi ya 65
 • Una mfumo dhohofu wa kinga ya mwili mfano sababu ya kisukari au kansa
 • Una matatizo ya moyo mapafu na figo

It is how you want it to Be. Always!

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.