Fahamu sababu kuu za kutapika kwa watoto.

Je kutapika ni nini?

Kutapika ni hali ya mtu au mnyama kutokwa kwa nguvu na vitu vilivyojikusanya tumboni kupitia mdomoni na wakati mwingine puani.

Ni kawaida kwa watoto wachanga na watoto kutapika. Katika kesi nyingi, kutapika hudumu kati ya siku moja mpaka mbili na si ishara ya kitu chochote kikubwa.

Visababishi vya kutapika kwa mtoto.

Mtoto mdogo anawezakutapika kutokana na sababu mbalimbali. Baadhi ya sababu hizi ni;

  1. Mambukizi katika mfumo wa chakula (Gastroenteritis): Maambukizi haya kwa kawaida husababishwa na aidha bakteria au virusi. Kwa kawaida mfumo wa kinga ya mtoto hupigana na maambukizi baada ya siku chache.
  2. Kumeza hewa wakati mtoto anapokula: Hii hutokea mara nyingi hasa pale ambapo mtoto anapokua analishwa na mtoto huyu akameza hewa.
  3. Maambukizi hatari: Watoto wadogo wapo katika hatari kubwa ya maambukizi hatarishi kama maambukizi ya njia ya hewa kama maambukizi ya homa ya mapafu (pneumonia). Fahamu kuhusu maambukizi ya ugonjwa huu kupitia link ifuatayo:http://daktarimkononi.com/2018/06/24/homa-ya-mapafu-kwa-watoto-pneumonia-in-children/
  4. Dalili ya magonjwa hatari: Endapo mtoto ataendelea kutapika mfulululizo huashiria maambukizi ya magonjwa hatari kama homa ya uti wa mgongo. 

Nini cha kufanya?

Hakikisha mtoto wako anakunywa maji na vyakula au matunda yenye asili ya maji maji kwa wingi ili kurudisha maji yaliyopotea mwilini. 

Endapo mtoto ataendelea na hali ya kutapika ni vyema kumuwahisha hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi. Mtoto anaetapika anatakiwa kumuona daktari endapo;

  • Anatapika zaidi ya masaa 24
  • Mtoto wako anatapika ndani ya masaa nane na unahisi ana upungufu  wa maji mwilini.
  • Ana maumivu makali ya tumbo.
  • Ana maumivu makali ya kichwa na shingo iliyo kakamaa.
  • Anagoma kula, yupo katika hali ya unyong’onyevu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center