Tabia hatarishi zinazoweza kusababisha upoteze ujauzito wako

Mimba(ujauzito) nikipindi cha week kati ya 37 mpk 42 au zaidi ambapo mtoto huishi ndani ya tumbo la uzazi la mama. Katika kipindi hiki kwa kiasi kikubwa maisha ya mtoto hutegemea sana maisha anayoishi mama mzazi, hvyo endapo mama ataishi maisha hatarishi basi kuna uwezekano mkubwa kabsa wa mtoto kuathirika au kupoteza maisha!

Kuna baadhi ya tabia ambazo tunazifanya kama sehemu ya utamaduni wetu lakini kwa namna moja au nyingine zinaweza kusababisha ukapoteza ujauzito wako (mimba kuharibika).

Tabia hatarishi zinaweza pelekea kupoteza ujauzito

Katika jamii yetu tumekua na mazoea ya kutumia dawa kwa mazoea kulingana na shida mbali mbali tunazozipata bila hata kupata ushauli kutoka kwa daktari, tabia hii ni mbaya sana wakati wa ujauzito kwa sababu kuna baadhi ya dawa haziruhusiwi kabisa kutumiwa kipindi hiki. Endapo zitatumika kipindi hiki zinaweza kuingilia na hatua za ukuaji wa mtoto na hatimae kusababisha kuharibika kwa mimba au mtoto kuzaliwa akiwa na upungufu wa maumbile. Baadhi wa dawa zinazozuiliwa kutumika kipindi cha ujauzito ni metronidazole(fragly), indomethasine, diclofenac, warfallin, artisunate na zingine nyingi  hivyo katika kipindi hiki ni muhimu sana kuongea na daktari kabla ya kutumia dawa yoyote ile.

Jamii ya watu wengi tumezoea kutopata matibabu ya magonjwa mbali mbali kwa kile kinacho aminika kwamba, miili yetu inakinga ya kutosha hivyo sio lazma kupata huduma ya kitabibu, tabia hii sio nzuri kipindi cha ujauzito kwani kuna baadhi ya magonjwa yasipotibiwa kikamilifu huweza kupenya na kuingia kwa mtoto na hivyo kuingilia suala zima la ukuwaji wa mtoto hvyo kusababisha kifo kwa mtoto au kupata mtoto kwenye mapungufu ya kumaumbile.  Magonjwa kama : magonjwa ya zinaa, malaria , toxoplasmosis, virusi vya rubella yana uwezo wa kupenya moja kwa moja kwa mtoto na kusababisha shida hii. Lakini pia magonjwa kama malaria, maambukizi katika njia ya mkojo( UTI), PID na mengine mengi husababisha joto la mwili kupanda mara kwa mara kitu ambacho sio kizuri katika kipind hiki cha mimba kwani kupanda kwa joto la mwili huambatana na mwili kuzalisha kemikali ziitwazo postaglandins ambazo huweza kusababisha mimba kuharibika.

Kwa jamii yetu dawa za miti shamba imekua kama njia mbalada ya tiba kwa magonjwa yetu, katika kipindi cha ujauzito tabia hii sio nzuri kwa sababu dawa hizi za miti shamba.. hazijafanyiwa utafiti wa kutosha ili kujua km zina madhara kwa mtoto wa tumboni au laa!!. Hivyo ni vizuri kutotumia kabsa kwani kinga ni bora kuliko tiba. Ukipata shida yoyote katika kipindi hiki cha ujauzito ni muhimu sana kumuona daktari kuliko kuchukua maamuzi mkononi ya kuanza kujitibia.

Pombe na sigara vyote vina kemikali ambazo zina uwezo wa kupenya moja kwa moja mpaka kwa mtoto na kuharibu mfumo mzima wa ukuwaji na uumbaji wa mtoto, hivyo kunaweza kusababisha kupoteza uhai wa mtoto au kupata mtoto kwenye mapungufu ya maumbile. Hivyo inashauriwa sana hata kama unavuta sigara au kutumia pombe basi kuacha kabisa kipindi hiki cha ujauzito kwa ajiri ya afya ya mtoto pamoja na mama.

Kipindi cha ujauzito ni kipindi kinachohitaji upungufu wa akili na mwili. Hivyo mama anashauriwa kupata muda wa kutosha wa kupumzika , kutojihusisha na kazi ngumu kupita kiasi pamoja na kuepuka ugomvi kwani vitendo hivi vinaweza athiri afya ya mama au mtoto au wote kwa pamoja.

Vifo vingi vya mama au watoto au wote kwa pamoja huzuiliwa kwa mama tu kuhudhuria kliniki kwa wakati, wakati wa kliniki kuna huduma muhimu sana zinatolewa kwa mama mjauzito ikiwemo pamoja na kupewa chanjo mbali mbali na dawa za kutibu na kujikinga na magonjwa hatarishi kwa afya ya mama na mtoto. Lakini pia mama hupimwa na kujua kama ana magonjwa yoyote na tiba yake huanza mara moja.

Www.daktarimkononi.com

4 Comments

 1. Warfarin
  Indomethacin
  Artesunate
  Flagyl
  Na pia Artesunate injection is safer options for treatment of severe malaria in pregnancy go and read about that.
  Thanks.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.