UMUHIMU WA WANAUME KUSHIRIKI KATIKA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI (Part 1)

Kuna jitihada nyingi za kumshirikisha mwanaume katika masuala ya afya ya uzazi zinzofanywa na serikali na mashirika binafsi ya kitaifa na kimataifa. Mojawapo ni mikakati ya kupanga sera zitakazoshawishi na kuvutia mwanaume katika huduma ya afya ya uzazi ikiwemo kuhudhuria kliniki ya uzazi pamoja na mwenza wake.

Ushiriki wa wanaume katika huduma za afya ya uzazi ni jambo la muhimu sana na linawekewa msisitizo sana sababu zifuatazo;

WAKATI WA UJAUZITO

  1. Kumpatia lishe bora mjamzito ili kuhakikisha uzazi salama wenye afya njema
  2. Mwanaume hua mstari wa mbele kumpeleka mwenza wake hospitali pindi anapoona dalili hatarishi na hivyo dalili hizi hutambulika akiwa ameshirikishwa vyema katika afya ya uzazi.

WAKATI WA KUJIFUNGUA

  1. Mama hupata msaada wa maandalizi muhimu kwa ajili ya kujifungua ikiwemo kuweka akiba ya fedha kwa mahitaji ya siku ya kujifungua na siku baada ya hapo.
  2. Mwanaume huusika vizuri katika maamuzi mengi katika kipindi hiki kupanga usafiri, kupanga muuguzi atakaemsaidia mama katika kujifungua na ulipaji wa huduma.

WAKATI BAADA YA UZAZI

  1. Mwanaume huusika kuhimiza afya bora kwa mama kwa kumpa muda wa kupumzika baada ya uzazi kwa kusaidia kazi ndogondogo za nyumbani huku akihimiza unyonyeshaji wa mtoto.
  2. Mwanaume anatakiwa kupanga na mwenza wake kuhusiana na uzazi na kukubaliana njia zipi za kutumia ili kuacha nafasi kati ya uzazi mmoja na mwingine
  3. Maamuzi mengi juu ya utarari wa kupima afya, uhiari wa kupima afya, kupata matibabu na gharama zake hufanywa na mwanaume hivyo basi ni jambo la msingi kumshirikisha mwanaume katika sekta ya afya ya uzazi.

TUJIULIZE

Je ni njia zipi zinazotumika kuhamasisha wanaume katika kushiriki katika huduma za afya ya uzazi?

Je tumefanikiwa kwa kiwango gani hadi sasa katika uhamasishaji wa wanaume kushiriki katika huduma za afya ya uzazi?

Tusikose kufuatilia nakala zetu za afya kwa majibu na kuelimika zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center