Fahamu kuhusu kisukari cha mimba na madhara yake.

Kama ilivyo kwa tatizo la kisukari, pia kisukari cha mimba ni tatizo ambalo huwapata baadhi ya wanawake wakati wa kipindi cha ujauzito, tatizo hili hupelekea kiwango cha sukari kuongezeka katika damu wakati wa ujauzito kutokana na homoni ya insulini kushindwa kufanya kazi vizuri,tatizo hili huweza kuleta athari kwa mama na mtoto endapo kiwango cha sukari hakitadhibitiwa.

Kwa kawaida wanawake wanaopata tatizo la kisukari wakati wa ujauzito hurudi katika hali ya kawaida baada ya kujifungua.

Visababishi vya kisukari cha mimba.

Kwa kawaida mwili wa binadamu huzalisha homoni iitwayo insulini ambayo kazi yake kubwa ni kupunguza kiwango cha sukari katika damu hivyo kuruhusu sukari itumiwe na mwili.

Wakati wa ujauzito kuna homoni maalum kama vile projesteroni na estrojeni ambazo huzalishwa kwa wingi wakati wa ujauzito, homoni hizi hupunguza kwa kiasi kikubwa utendaji kazi wa homoni ya insulini hivyo kupelekea kiwango cha sukari kwenye damu kupanda hali ambayo huweza kuathiri maendeleo ya ukuaji wa mtoto na pia huweza kuathiri afya ya mama.

Vihatarishi vya kisukari cha mimba.

Mwanamke yeyote anaweza kupata kisukari cha mimba, lakini wanawake ambao wako katika hatari kubwa ya kupata kisukari cha mimba ni wale ambao wana;

 • Umri wa zaidi ya miaka 25 wakati wa kupata ujauzito
 •  Historia ya tatizo la kisukari katika familia endapo tatizo la kisukari limekuwa likisumbua baadhi ya wanafamilia au wewe mwenyewe una tatizo la kisukari kabla ya kupata ujauzito hivyo hatari ya kupata kisukari cha mimba huwa kubwa zaidi.
 • Uzito mkubwa kupita kiasi, uzito mkubwa kupita kiasi wakati wa ujauzito huongeza hatari ya kupata kisukari cha mimba.

Dalili za kisukari cha mimba
Kwa kawaida kisukari cha mimba hakina dalili hivyo huwa vigumu kutambua kama mama mjamzito ana tatizo hili, lakini kupima mara kwa mara kiwango cha sukari katika damu wakati wa ujauzito huweza kugundua tatizo.

Madhara ya kisukari cha mimba kwa Mama na mtoto

 • Kujifungua mtoto mwenye uzito mkubwa, kiwango kikubwa cha sukari katika damu hupelekea mtoto kukua na kuwa uzito mkubwa ambao huweza kufikia mpaka kilo 4, hii huweza kubabisha matatizo wakati wa kujifungua kama vile kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.
 • Kujifungua kabla ya muda au mtoto kuzaliwa na matatizo ya upumuaji (respiratory distress syndome)
 • Kujifungua mtoto mwenye kiwango kidogo cha sukari, kutokana na uzalishaji mkubwa wa homoni ya insulini kiwango cha sukari huweza kuwa chini sana mara tu baada ya kuzaliwa hivyo kuweza kusababisha kifo cha mtoto baada ya kuzaliwa.
 • Mama huwa katika hatari kubwa ya kupata kisukari hata baada ya mimba( type 2 Diabetes).
 • Mama huwa katika hatari kubwa ya kupata shinikizo kubwa la damu au kifafa cha mimba.

Je nifanye nini kupunguza hatari ya kupata kisukari cha mimba.

Mama mjamzito anaweza kupunguza hatari ya kupata kisukari cha mimba kwa kuzingatia yafuatayo;

 • Kula matunda na mbogamboga kwa wingi jitahidi kuepuka kutumia kwa wingi vyakula vya wanga na mafuta.
 • Jiwekee ratiba nzuri ya kufanya mazoezi kabla na baada ya kupata ujauzito.
 •  Epuka kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi.

 

1 thought on “Fahamu kuhusu kisukari cha mimba na madhara yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show