Kwanini ni lazima mjamzito kwenda kliniki?

Ujauzito ni kipindi maalumu cha wiki kati ya 37 mpaka 42 au zaidi, ambapo mama huishi na mtoto wake ndani ya nyumba yake ya uzazi. Ni kipindi kinachohitaji uangalizi wa hali ya juu kwani vitu hatarishi vikitokea huweka hatarini maisha ya wote wawili mama na mtoto.

Katika kipindi cha ujauzito mama hupaswa kuchukua tahadhari mbalimbali lakini pia kua karibu sana na huduma za afya kwa ajiri ya kufuatilia kwa ukaribu afya ya mama na mtoto, hivyo katika kipindi hiki mama hutakiwa kuhudhuria kliniki kwa atakavyopangiwa na mtaalamu wake wa afya! 

Ni muhimu sana kwa mama mjamzito kuhudhuria kliniki, kwa sababu kuna huduma muhimu sana anazopatiwa ili kudumisha afya kwake na mtoto wake,  lakini kuzuia vifo visivyokua vya lazima kwa mama na mtoto, baadhi ya huduma zinazotolewa kliniki ya mama mjamzito ni pamoja na;

  1. Kupimwa afya ya mama.  Kipindi cha ujauzito mama hupimwa afya na magonjwa mbali mbali kama vile malaria, HIV, kaswende, homa ya ini na mengine mengi. Ni muhumu sana kufanya hivi kwa sababu baadhi ya magonjwa kama malaria, toxoplasmosis, virusi vya rubella, kaswende na magonjwa mengine ya zinaa yanaweza kupenya na kwenda kwa mtoto hivyo kuathiri ukuaji wa mtoto hata kusababisha mimba kuharibika au kupata mtoto mwenye mapungufu kimaumbile. Hivyo mama hupimwa na kutibiwa magonjwa haya kama akikutwa anayo. Lakini pia kupima HIV ni muhimu sana kwani kama mama akikutwa ana HIV basi ataanza moja kwa moja kutumia ARV lakini pia kuna huduma atapatiwa ili kuongeza uwezekano wa kupata mtoto asiye na virusi vya ukimwi.
  2. Tiba za awali. Wakati wa kliniki mama hupatiwa vidonge vya kuongeza damu kwa sababu wajawazito wengi hupata tatizo la upungu wa damu kitu ambacho ni hatari kipindi hiki cha ujauzito, hivyo wakati hu wa ujauzito mama hupatiwa vidonge kama multivitamin tablets kwa ajiri hiyo, lakini pia hupatiwa folic acid tablets(vidonge) kwa ajiri ya kuzuia kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, mbali na hapo pia hupatiwa vidonge vya SP kwa ajiri ya kinga ya malaria kali kaa mama mjamzito.
  3. Chanjo ya magonjwa mbali mbali.  Mama aendapo kliniki pia hupaitwa chanjo ya magonjwa mbali mbali kama vile chanjo ya homa ya ini na chanjo ya tetenasi, chanjo hizi ni muhimu kwani humkinga mama kupata magonjwa ambayo ni hatarishi kwa mtoto!
  4. Kupimwa shinikizo la damu (blood pressure) na mkojo. Wakati wa ujauzito mama hufanyiwa vipimo hivi na ni muhimu kwa sababu huweza kugundua dalili za awali za ugonjwa wa kifafa cha mimba (pre eclampsia anda eclampsia), hivyo kuanza kuchukua tahadhari za awali na tiba!
  5. Elimu juu ya umuhimu wa mazoezi na chakula kinachofaa. Wakati wa ujauzito ni kipindi pia muhimu kwa ajiri ya kuvunja mila potofu juu ya aina ya vyakula anavyopaswa kula mama mjamzito. Kuna mila potofu kama kula mayai kipindi cha ujauzito husabisha kupata mtoto asiyekua na nywele, hii mila ni ya uwongo. Ni muhimu sana kula vyakula aina ya protini kipindi cha ujauzito na aina zingne za vyakula kutokana na hali ya mama. Pia elimu ya mazoezi na umuhimu wake wakati wa kliniki.
  6. Huduma ya utrasound. Pia kwa vituo vya afya vilivyo endelea, mama hutakiwa kupima walau mara moja ili kujua mtoto amekaaje, kama anatatizo lolote lakini pia kujua jinsia ya mtoto kama ni wa kiume au kike.

Vifo vingi vya mama na watoto huzuiliwa kwa mama mjamzito kuhudhuria kliniki ladiri ya ratiba yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center