Je, wataka fahamu jinsi ya kuondoa makovu na kuzuia chunusi mpya!?

UTANGULIZI

Wengi hujiuliza kama kuna tiba ya chunusi, kwa kumaanisha dawa au njia ambayo inaweza kutumika kumaliza chunusi kabisa. Kiukweli hamna tiba ambayo inaponya chunusi kabisa lakini kuna tiba zilizopo kwa ajili ya kupunguza athari na kupunguza makovu katika ngozi kutokana na chunusi.
Matibabu ya chunusi yanajikita katika kuzuia chunusi mpya, chunusi na mabaka ambayo yalikuwepo kabla ya kuanza matibabu huisha taratibu ndani ya wiki au miezi kadhaa. Kulingana na wingi wa chunusi mabadiliko ya maana huanza kuonekana baada ya miezi miwili hadi miezi nane.

Fahamu ya kwamba...

Malengo makubwa ya hizi tiba ni kumpunguza kujisikia vibaya kutokana na maumivu ya chunusi, kuboresha mwonekano wa ngozi, kuzuia makovu pamoja na kupunguza matatizo ya kisaikolijia kutokana na mtazamo wa jamii juu ya chunusi.

Mambo ya kuzingatia katika kutibu na kuzuia chunusi!

Hupaswi kushika shika na kutumbua chunusi kwani hii huongeza uwezekano wa kuweka vijidudu mbali mbali usoni ambavyo vinaweza kuzidisha zaidi chunusi na kusababisha mabaka.

Ni muhimu kuosha uso mara mbili kwa siku kwa kutumia maji ya uvugu vugu na sabuni. Vile vile kutumia mild facial cleanser baada ya kuosha uso ili kuhakikisha ngozi ni safi kabisa. Kuosha uso mara kwa mara au kwa kutumia nguvu sana haishauriwi kwani inaweza kuleta madhara zaid kwa ngozi.

 Inashauriwa kutumia mosturiser ambayo haina mafuta (oil free moisturiser) yenye kinga ya jua (spf 15 na kuendelea). Epuka vipodozi vyenye mafuta(Oil based)

Kwa kumalizia...

Aina ya matibabu ya chunusi inategemea sababu na wingi wa chunusi. Ni muhimu kumuona daktari wa ngozi ili kuweza kupata matibabu yanayoendana na chunusi zako. Ni muhimu kufahamu kuwa chunusi haziponi, lakini matibabu yanapunguza au kudhibiti kabisa chunusi mpya hivyo mara nyingi muathiriwa atahitajika kujali ngozi yake siku hadi siku bila kuchoka hata baada ya kumaliza matibabu ili kuzidi kuwa na uso bila chunusi.


BUTAMO, January J. MD4 🇹🇿

MEDICAL STUDENT|DMer|Entrepreneur|Tech enthusias|Aspiring Surgeon

All author posts

Privacy Preference Center