Mimba zaidi ya miezi 9 bila kujifungua! Sababu ni nini??

Mimba ni kipindi za wiki kati ya 37 mpaka 42 ambapo mtoto huishi ndani ya nyumba ya uzazi ya mama, ambapo kwa kipindi hiki mtoto hukua na humtegemea mama kwa kila kitu!

Mtoto hawezi kukaa ndani ya nyumba ya uzazi ya mama milele, kuna muda ambapo mtoto ni lazima atoke nje na aanze kujitegemea yeye kama yeye! Kwa kawaida mtoto huishi kwa muda wa wiki 37 mpaka 42 ndio anazaliwa!.. ila kuna wakati mtoto anaweza kuzaliwa kabla au baada ya huo muda kutokana na sababu mbali mbali!,

Sababu zipi hufanya mimba kukaa zaidi ya miezi 9 bila kujifungua??

Sababu zinazofanya mtoto kuzaliwa baada ya muda tarajiwa (baada ya wiki 42) mpaka sasa hazijulikani, hali hii inaweza kua ya kawaida kwa baadhi ya watu au pia ikawa ni ishara ya tatizo kwa baadi ya watu pia! Tafti za kisayansi zinasema kuna baadhi ya mambo humuweka mama katika hatari ya kupata mtoto baada ya wiki 42, mambo hayo ni;

  • Historia ya familia kua na tatizo hili, au pia mama kama alizaliwa kwa hali ya kuchelewa, hali hii humuongezea mama hali ya kupata tatizo hili.
  • Mimba ya kwanza kwa mama
  • Mama akiwa mnene kupita kiasi
  • Mtoto akiwa na matatizo/ upungufu wa kimaumbile
  • Pia endapo mama atakosea kuhesabu siku zake, anaweza kudhani muda umepita likini ikawa bado, kwa hali kama hii utrasound hutakiwa kufanyika ili kupata umri sahihi wa mimba!

Je kuna madhara yoyote kwa mama na mtoto endapo mimba itakaa zaidi ya miezi 9??

Kwa sehemu kubwa hali hii huwa ni ya kawaida, ila mama hutakiwa kwenda kliniki kwa ajiri kuchinguzwa ili kujua kama ni hali ya kawaida au lah!! Kuna baadhi ya matatizo huwapata watoto wanaokaa zaidi ya miezi 9 ndani ya nyumba ya uzazi;

  • Huongeza hatari ya mtoto kufika tumboni
  • Mtoto anaweza kukua, akawa na umbo kubwa na uzito zaidi ya kilo 4.5kg (macrosomia) big baby! Hivyo kusababisha shida wakati wa kujifungua!
  • Mtoto anaweza kunywa maji machafu (meconium aspiration) hivyo kusababisha mtoto kupata shida ya kupumua!
  • Pia mama anaweza kupata matatizo kama uchungu wa muda mrefu( prolonged labor) hivyo kujifungua kwa upasuaji, maumivu ya tumbo la chini!, pia hatari ya maambukizi na kuumiza viungo vya karibu.

Je nini kifanye endapo mama atapata hali hi??

Endapo mama atakaa zaidi ya miezi 9 bila kujifungua.. anashauliwa kumuona daktari ili kunguzwa na kujua kama hali hiyo ni ya kawaida au ni tatizo… na utapewa huduma stahiki kulingana na tatizo lako!!

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show