Fahamu kuhusu tatizo la udhaifu wa mifupa (osteoporosis).

Tatizo la udhaifu wa mifupa lijulikanalo kitaalamu kama osteoporosis ni tatizo ambalo huwakumba zaidi wanawake hasa wale ambao wamefika katika umri wa hedhi kusimama. Wanaume pia wanaweza kupata tatizo hili la udhaifu wa mifupa.

Tatizo la osteoporosis hupelekea mifupa kuwa laini sana na dhaifu hivyo huweza kuvunjika kirahisi hasa katika maungio ya kiganja cha mkono, uti wa mgongo ,nyonga na mifupa ya paja.

Dalili za tatizo la udhaifu wa mifupa.

Tatizo hili ni hatari kwani mara nyingi huwa halionyeshi dalili mapema hadi pale ambapo tatizo linakuwa limeshakuwa kubwa ambapo mtu huweza kupata dalili zifuatazo:

 • Maumivu makali ya mifupa hasa katika maeneo ya nyonga na uti wa mgongo.

 • Kupungua urefu kwa kiasi fulani kutokana na mifupa kushindwa kuhimili uzito wa mwili.
 • Mifupa kuvunjika kwa urahisi kupita kawaida. Mfupa hata huweza kuvunjika kutokana na kuanguka baada ya kujikwaa.
 • Kuwa na mkao ambao si wa kawaida (stooped posture).

Je, Nini husababisha tatizo hili?

Kwa kawaida mifupa ya binadamu huwa ipo katika mchakato endelevu ambapo seli za mifupa hutengenezwa na kuharibiwa. Ili mfupa uweze kukua mchakato wa kutengeneza seli za mifupa huwa zaidi ya mchakato wa kuziharibu seli hizi.

Lakini mtu mwenye tatizo la osteoporosis mchakato wa kuharibu seli za mifupa huwa zaidi ya mchakato wa kutengeneza seli hivyo kupelekea mfupa kuwa dhaifu.

Mambo yanayoweza kupelekea tatizo la osteoporosis.

Vihatarishi ambavyo huongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo la osteoporosis ni pamoja na;

 • Jinsia na umri- wanawake hasa wale ambao wana umri mkubwa wako katika hatari  kubwa ya kupata tatizo la osteoporosis ukilinganisha na wanaume.
 • Kiwango cha homoni- kupungua kwa homoni za kike hasa homoni ya estrojeni kwa wanawake ambao hedhi ilishasimama hupelekea kwa kiasi kikubwa tatizo la osteoporosis. Pia kwa wanaume kupungua kwa homoni ya testosteroni huchangia kutokea kwa tatizo hili kwa wanaume. Pia kuongezeka kwa kiwango cha homoni ya thyroidi kwenye damu huweza kupelekea tatizo la osteoposis.
 • Matumizi ya baadhi ya madawa ya pumu kwa muda mrefu.
 • Kupungua kwa kiwango cha madini ya chokaa (calcium)- kupungua kwa madini ya chokaa mwilini kutokana na kutokula vyakula vyenye madini haya au kutokana na kuwa matatizo katika mfumo wa chakula hivyo kushindwa kusharabu madini haya, huweza kupelekea tatizo la osteoporosis.
 • Matumizi ya pombe na sigara yaliyokithiri.

Madhara ya tatizo hili.

Kwa sababu tatizo hili la wepesi wa mifupa hupelekea mifupa kuvunjika kwa urahisi, mivunjiko hii huweza kupelekea ulemavu au wakati mwingine kifo endapo mifupa ya uti wa mgongo ikaharibu mfumo wa fahamu baada ya kuvunjika.

Kinga na tiba.

Tiba ya tatizo la osteoporosis hutolewa baada ya uchunguzi wa kina kubaini kisababishi cha tatizo hili, hivyo unapopata dalili zozote ambazo zinaelekeana na dalili za tatizo hili basi ni vyema kuwahi hospitali kwa uchunguzi zaidi na tiba.

Lakini kwa yale makundi ambayo yako katika hatari ya kupata tatizo la osteoporosis yafuatayo yanaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kupata tatizo la osteoporosis.

 • Kula vyakula vyenye madini ya chokaa kwa wingi- vyakula jamii ya mbogamboga, maziwa, samaki na soya ni vyanzo vizuri vya madini ya chokaa.

 • Kuwa na tabia ya kuotea jua la asubuhi au jioni kwani husaidia mwili kutengeneza vitamin D ambavyo husaidia mwili kusharabu madini ya chokaa  ambayo ni muhimu katika utengenezaji wa mifupa.
 • Fanya mazoezi ya viungo kuimarisha mifupa yako.

3 thoughts on “Fahamu kuhusu tatizo la udhaifu wa mifupa (osteoporosis).

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show