Ninafanya diet lakini sipungui,Je tatizo ni nini?

Watu wengi wamekuwa wakikumbana na hili tatizo la kufanya diet lakini bado wakirudi kupima uzito kwenye mizani mambo huwa ni yale yale au hata kuwa mabaya zaidi.

Makala ya leo itakuonyesha juu ya ulaji ulio wa afya na pia ulio sahihi kukusaidia kupunguza uzito wako.

1.kutoruka mlo wa asubuhi(breakfast)

Wengi wetu tumejikuta tukimaintain kwa kuruka breakfast na baadae kujikuta tukifidia ule mlo kwa kula chakula hata kingi zaidi

2.muda wa kula

Muda mzuri wa kula ni masaa manne baada ya kuamka,mchana na masaa takribani matatu kabla ya kulala,hii huupa mwili wako mda wa kukimen’genya chakula vizuri na kuyeyusha mafuta yaliyopo kwenye chakula

3.aina ya chakula

Aina ya vyakula sahihi tunavyopaswa kula ni vyakula vyenye protein kwa wingi,mboga za majani na matunda kwa wingi pia ,wanga kidogo bila kusahau unywaji maji ya kutosha.

4.kutokuwa na msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo au stress hupelekea kula vyakula ambavyo sio sahihi kwa afya yako na kwa wingi kama vile pombe, snacks mfano crips,biskuti,pipi,chocolate na kadhalika hata hivyo mwili huhifadhi mafuta kwa wingi kipindi ukiwa na stress

5.kupata usingizi wa kutosha

Inashauriwa kulala masaa 6 hadi 8, kwani Kutopata usingizi wa kutosha hufanya mwili wako kumen’genya chakula taratibu .

Lakini pia diet tu haitoshi mazoezi nayo ni muhimu katika kupunguza uzito,hakikisha unafanya mazoezi walau mara tatu hadi nne kwa week kwa muda wa dakika 20 hadi 30.

 

8 thoughts on “Ninafanya diet lakini sipungui,Je tatizo ni nini?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show