FAHAMU KUHUSU UGONJWA SUGU WA FIGO (CHRONIC KIDNEY DISEASE)-SEHEMU YA KWANZA

UTANGULIZI.

Ugonjwa sugu wa figo ni nini?

Ugonjwa sugu wa figo ni hali ya figo kudhoofika kwa muda mrefu wa miezi au miaka na kusababisha figo  kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha. Mtu mmoja kati ya watu kumi ana aina fulani ya ugonjwa wa figo usiopona.

Kwa wagonjwa walio wengi figo hazishindwi kabisa kufanya kazi lakini uwezo wake hupungua kwa kiasi. Hivyo basi kufeli kwa figo sio kushindwa kabisa kufanya kazi yake.

Ni wakati gani figo figo hufeli kabisa?

Figo husemekana kuwa zimefeli na kufikia ukomo wa kazi yake pale ambapo uwezo wake hupungua hadi kufikia asilimia kumi(10%) ya uwezo wa kawaida. Figo zinapofikia hatua ya kufeli kabisa huwa haziwezi kupona kwa matibabu ya kutumia dawa bali huhitaji kubadilishwa au kufanyiwa dayalisisi ili mtu aweze kuendelea kuishi.

 

Nini chanzo cha ugonjwa sugu  wa figo?

Kuna mambo mengi ambayo huweza kusababisha ugonjwa sugu wa figo na kusababisha madhara ambayo yanaweza yasitibike lakini vyanzo vikubwa vikuu ni ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu . Kisukari na shinikizo kubwa la damu huchaingia zaidi ya asilimia sabini na tano( 75%) ya ugonjwa sugu wa figo.

Sababu kuu za ugonjwa sugu wa figo ni:

1.Kisukari:

Kisukari ndicho chanzo kikubwa cha ugonjwa sugu wa figo. Zaidi ya asilimia arobaini na tano(45) ya magonjwa ya figo yasiyopona husababishwa na kisukari. Kati ya watu watatu hadi watano wenye kisukari mmoja huweza kupata ugonjwa sugu wa figo.

2.Shinikizo kubwa la damu:

Shinikizo la damu lisipotibiwa au kudhibitiwa kwa njia zifaazo huweza kuwa chanzo kikubwa cha ugonjwa wa figo. Zaidi ya asilimia thelathini ya magonjwa sugu ya figo husababishwa na shinikizo kubwa la damu ambalo halikutibiwa. Shinikizo kubwa la damu pia  huzidisha madhara kwenye figo ambazo zimeshaathiriwa na hali nyingine.

3.Sababu nyingine:

  • Ugonjwa wa uvimbe kwenye figo,
  • Ugonjwa wa figo wa polisisitiki,
  • Kufunga kwa mishipa iendayo kwenye figo,
  • Mkojo kuzuiwa na mawe yaliyopo kwenye figo au ugonjwa wa tezi dume uliopo karibu na kibofu,
  • Figo kuzeeka,
  • Mtumizi ya dawa fulani fulani kwa muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.