MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA (DYSPAREUNIA) YATOKANAYO NA MAAMBUKIZI YA VIA VYA UZAZI (PID)

Maumivu yatokanayo na maambukizi ya mfumo wa uzazi huweza kuwapata Mwanawake wa umri wowote hasa walio katika umri wa kuzaa (sexually active).

Maambukizi hayo hutokana na vimelea (bacteria) hasa wa kisonono (Neisseria gonorrheae) na pangusa (Chlamydia trachomatis) , Magonjwa sugu ya njia ya mkojo (chronic UTI). Vimelea hawa husambazwa kwa njia ya kujamiiana bila kinga au ngono isiyo salama.

Maumivu wakati wa tendo la ndoa hupelekea kuharibika kwa mahusiano baina ya wenza.

Huchangia katika kueneza maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

Maumivu wakati wa tendo la ndoa hupunguza hamu ya tendo.

 

VISABABISHI VINGINE VYA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA

Mambo mengine yanayoweza kusababbisha maumivu wakati wa tendo la ndoa ni kama;

  • kupungua au kukauka kwa ute ukeni
  • ukomo wa hedhi
  • kushiriki tendo la ndoa mara tu baada ya kujifungua
  •   maambukizi ya magonjwa katika via vya uzazi
  •   matatizo ya kisaikoloji

NIFANYEJE NIKIWA NA TATIZO LA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA?

  1. Kwa mwanamke anayepata maumivu anashauriwa kumuona daktari kwa ajili ya kufanya uchunguzi zaidi.
  2. Kufanya matibabu kikamilifu ya maambukizi ya via vya uzazi.
  3. Unashauriwa kuepuka ngono isiyo salama na utoaji mimba usio salama kwani huchochea kusambaa kwa maambukizi ya uzazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center