NATAKA KUPUNGUZA UZITO BILA KUFANYA MAZOEZI,JE INAWEZEKANA?

Asilimia   yetu  kubwa tunataka  kupungua  lakini  mazoezi  huwa  ni kikwazo kwetu  kutokana  na majukumu tuliyonayo au ukosefu wa msukumo  ndani yetu  wa kufanya mazoezi.

Zifuatazo ni njia za kupunguza uzito pasipo kufanya mazoezi.

1.kula chakula chenye protini kwa wingi

Protini katika mwili hufanya kazi ya  kusaidia homoni  zinazoshibisha  na kukufanya ukinai  kwa haraka ,hivyo  kupunguza njaa na hukufanya ule chakula kidogo,mfano wa vyakula venye protini ni kama vile mayai,samaki,maziwa,nyama,jamii ya kunde kama vile soya,maharage

2.kunywa maji mara kwa mara

Haswa kabla ya mlo wako,hii husaidia ule chakula kidogo ,vilevile pendelea kunywa maji yenye uvugu vugu haswa unapoamka asubuhi.Maji ya uvuguvugu huongeza joto mwilini na  kuongeza kasi ya kumeng’enya chakula  hivyo kupunguza mafuta mwilini,hatimaye na uzito kupungua pia.

3.Hakikisha unatafuna  chakula chako vizuri  na kwa  taratibu

Ubongo wako unahitaji mda wa kutosha kukubali kwamba ulichokula kinakutosha na hauhitaji nyongeza,hivyo basi itakufanya ule kidogo na utosheke kwa haraka zaidi.

4.Pata usingizi wa kutosha na upunguze msongo wa mawazo

Inapokuja katika swala la afya ,wengi wetu huwa tunaweka usingizi na msongo wa mawazo pembeni.Hivi viwili vina nguvu kubwa katika  hamu ya chakula pamoja  na uzito.

Ukosefu wa usingizi  pamoja na usongo wa mawazo huingiliana na kazi za homoni zinazokupa hamu ya chakula ,na hivyo basi huongeza  hamu ya vyakula visivyo na afya,mbali zaidi hukuhatarisha na magonjwa yasioambukizwa.

5.Achana na  vinywaji venye sukari

Ni rahisi sana kuongeza uzito kupitia vinywaji venye sukari kwa maana ni vinywaji vya hamu tu,lakini zina kalori kubwa .

Ukweli ni kwamba kupunguza uzito  huchangiwa  kwa  kiwango kikubwa na mfumo wetu wa maisha haswa  mlo na asilimia ndogo na mazoezi.

 

5 thoughts on “NATAKA KUPUNGUZA UZITO BILA KUFANYA MAZOEZI,JE INAWEZEKANA?

  1. Asante kwa ushauri wenu mzuri, lakini pia naomba kufahamu kama ni salama kiafya kutumia ya uvugu vugu ya ukwaju au pia maji ya uvugu vugu yenye unga wa majani ya mlonge

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show