Fahamu kuhusu tatizo la kuharibika kwa mimba (miscarriage).

Kuharibika kwa mimba ni hali ya mimba kutoka ikiwa chini ya miezi mitano, ingawa mimba nyingi zinazoharibika huwa zinaharibika kabla ya hata kufikisha miezi mitano. Kutokana na mimba nyingi zinazoharibika kuharibika katika kipindi cha miezi ya mwanzoni ya ujauzito, baadhi ya wanawake huwa hawafahamu kuwa mimba imeharibika kutokana na kutokufahamu kama ni wajawazito.

Dalili za kuharibika kwa mimba.

Kama tulivyoona mimba nyingi huharibika zikiwa bado chini ya miezi mitano ya ujauzito. Zifuatazo zinaweza kuwa baadhi ya dalili na viashiria vya kuharibika kwa mimba:

 • Maumivu yanayouma kwa kuvuta hasa sehemu za chini za mgongo.
 • Kutoka damu nyepesi ukeni ambayo baadaye huwa nzito.
 • Homa
 • Uchovu

Je, husababishwa na nini?

Mara nyingi kuharibika kwa mimba husababishwa na mtoto kuwa na matatizo ya ukuaji wa kimaumbile hivyo kushindwa kuendelea kukua katika mfuko wa uzazi.

Visababishi vingine ni pamoja na;

 • Maambukizi mbalimbali wakati ujauzito, baadhi ya maambukizi haya hutokana na wanyama tunaoishi nao. Jifunze zaidi hapa.
 • Mama mjamzito kuwa na tatizo la kisukari.
 • Matatizo ya mfumo wa homoni.
 • Wakati mwingine hutokana na shingo ya kizazi (cervix) kushindwa kuhimili kubeba ujauzito kutokana udhaifu wa shingo ya kizazi (incompetent cervix).

Vihatarishi vya kuharibika kwa mimba.

 • Matumizi ya pombe na sigara kupita kiasi na madawa ya kulevya. 
 • Kuwa na magonjwa sugu kama vile kisukari.
 • Kuwa na umri mkubwa (zaidi ya miaka 35).
 • Matatizo katika mfumo wa uzazi.
 • Kuwa na historia ya mimba kuwahi kuharibika.

Ili kupunguza hatari ya mimba kuharibika ni vyema kuwa na tabia ya kuhudhuria kliniki mara kwa mara wakati wa ujauzito ili kupata msaada wa kitaalamu zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center