MTINDO WA MAISHA UNAVYOWEZA KUATHIRI NGUVU ZA KIUME KWA VIJANA

 1. Uume dhaifu kwa kitaalamu inaitwa Erectile dysfunction E.D au Impotence.Endapo mwanaume anashindwa kusimamisha uume,umekosa nguvu ya kutosha kuingia ndani ya uke na kushindwa kurudia tendo la ndoa baada ya kumaliza bao moja au kukojoa mara moja,huyu tunamuita anaupungufu wa nguvu za kiumekusimama kwa uume kunatokana na mapigo ya moyo kupanda baada ya mtu kupata ashki ya kufanya tendo la ndoa(sexual arousal),hivyo basi moyo husukuma damu nyingi kuelekea sehemu za uzazi ambayo damu hio huijaza mishipa midogo midogo ya damu(sponge like bodies)inayotengeneza uume(penis).
  DALILI ZA TATIZO HILI
  1.Kushindwa kusimamisha uume mara kwa mara.
  2.Uume kulala au kusinyaa katikati ya tendo la ndoa .
  3.Kushindwa kusimamisha ipasavyo.
  4.Kukojoa haraka mara baada ya kuanza kujaamiana au kukaa mda mrefu sana bila kukojoa.
  5.Maumivu ya misuli ya uume wakati wat endo la ndoa.

SABABU ZINAZOSABABISHA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME ZINAWEKWA KATIKA MAKUNDI MAWILI;
MATATIZO YA KIAFYA YA MWILI (ORGANIC CAUSES)
1.Magonjwa ya kisukari(diabetes mellitus.)
2.Ugonjwa wa presha (blood pressure)
3.Matatizo ya Tezi dume ,kama mtu amewahi fanyiwa operation (Prostatectomy surgery).
4.Upungufu au mvurugiko wa uzalishaji homoni za uzazi za mwanaume (hormonal insufficiencies/hypogonadism).
5.Athari za matumizi ya dawa kwa mda mrefu (Drugs side effects.)

Matatizo haya kwa pamoja hupelekea mishipa ya damu kuziba na mwishowe misuli inakosa nguvu za kuweza kusimama na hatimaye uume hisinyaa.
MATATIZO YA KISAIKOLOJIA (PSHYCHOLOGICAL PROBLEMS).
Mtu anaweza shindwa kusimamisha uume kutokana na matatizo ya kimawazo kama vile ;
1.Msongo wa mawazo (Stress).
2.Migogoro katika mahusiano.
3.Matatizo ya kimaisha,kukosa raha,kuwa na hasira.

4.Matatizo haya hupelekea wanaume wengi kukojoa kwa haraka sana hali ambayo haileti raha.

Lakini mda mwengine sababu ya uume mlegevu au dhaifu husababishwa na namna tunavyoishi kuanzia chakula tunachokula ,kazi tunazofanya ,mazoezi na kadhalika.
Je? Ni namna gani ya kuishi ni hatarishi kwa afya ya uzazi ya mwanaume yaani hupunguza nguvu za kiume na kufanya uume uwe dhaifu;
1.Lishe duni,kutokula mlo kamili au kula pasipo kufuata kanuni za lishe bora.Kwa mfano kupendelea kula aina Fulani tu ya vyakula kama vile wanga na mafuta na kuacha vyengine.
2.Uvutaji wa sigara(smoking),sigara ina sumu ya NICOTINE ambayo ni hatari katika mwili wa binadamu hasa kwenye mishipa ya damu.
3.Ulevi uliopitiliza,Kunywa pombe kupita kiasi pia huweza kuongeza tatizo la nguvu za kiume.
4.Msongo wa mawazo(Stress).
5.Migogoro na matatizo yote katika mahusiano.
6.Matatizo ya kisaikolojia (Psychological issues).

JINSI YA KUTIBU UUME DHAIFU KWA KUBADILI NAMNA YA KUISHI;
1.Kula mlo kamili kwa afya.Kula kwa wingi vyakula vya wanga au sukari na vyakula vya mafuta vinaweza sababisha kugandiana kwa mafuta ndani ya mishipa ya damu na kuleta matatizo ya moyo na kisukari,hii hupunguza usafirishaji wa damu kutoka kwenye moyo kwenda sehemu mbali mbali za mwili na kwenye uume pia hivyo uume hukosa nguvu na kushimdwa kusimama imara .Badili vyakula na anza kula matunda na mboga za majani kwa wingi bila kusahau kuwa na uzito ambao sio hatarishi kwa afya yako.
2.Fanya mazoezi mara kwa mara.Kuwa na tabia ya kufanya mazoezi angalau dakika 30 kila siku itakusaidia kuimarisha afya yako,kupunguza msongo wa mawazo,kuufanya mwili uwe na nguvu na sio legelege pia huimarisha usafirishaji wa damu katika mishipa ya damu kutoka kwenye moyo.
3.Acha uvutaji wa sigara.Kutokana na tafiti zilizofanywa mwanaume anaevuta sigara yupo kwenye hatari kubwa ya kupata matatizo ya uume dhaifu .Lakini wale wanaoacha mara moja uvutaji wa sigara kuna uwezekano wa kupunguza tatizo hilo kuliko wale wanaoendelea.
4.Jaribu kutatua na kuepuka matatizo ya msongo wa mawazo na migogoro ya mahusiano .Vyote hivi vina mchango mkubwa sana katika kulikamilisha tendo la ndoa na afya ya uzazi pia .Ongea matatizo yako kwa mpenzi au mwenzi wako au kwa daktari na watu wa ushauri na saha inaweza ikasaidia kutatua matatizo yenu.

Kuna matibabu mengi ya Uume dhaifu kutoka vituo vya afya ,lakini pia kubadili namna ya kuishi kunaweza kukawa na tiba na kinga nzuri sana ya tatizo hilo.
Ndugu yangu achana sasa na matumizi ya vidonge vya kuongeza nguvu za kiume(Viagra),maana baadaye hutaweza kabisa kusimamisha.

2 thoughts on “MTINDO WA MAISHA UNAVYOWEZA KUATHIRI NGUVU ZA KIUME KWA VIJANA

 1. 1. Je kifanyike nini endapo uume utalala baada ya tendo moja ili uweze kuendelea kufanya mapenzi na mwenzi wako???
  2.Ni kwanini wanawake walio wengi baada ya kujifungua hukaa muda mrefu bila kuona siku zao? pengine hili lina ukwel ndani yake?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center