Je, unajua sababu zinazopelekea kutapika damu? JIFUNZE NASI!

JE, UMEWAHI TAPIKA DAMU!?

Mfumo wa umeng’enyaji wa chakula ni mojawapo ya kati ya mifumo muhimu katika mwili wa mwanadamu kutokana na uwezo wake wa kubadilisha chakula kutoka katika mfumo wa mabongebonge na kuvunjavunja kuwa katika ukubwa unaoweza kufyonzwa na mwili.
 
Hitilafu hutokea katika mfumo huu na kupelekea dalili tofautitofauti ambayo mojawapo ni kuatapika chakula na vimengenyo vilivyo katika mfumo huu.
 
ukitaka kujua jinsi ya kuzuia kutapika BOFYA  hapo chini.

Maswali ya kujiuliza wakati wa una shida ya kutapika!

Jiulize!

Je, matapishi yana nini? damu?, chakula cha muda mrefu? ni maji tu? chakula chote nilichokula?

Jiulize!

Je, nina dalili zingine kama homa, maumivu ya tumbo, kuharisha, au kutoa haja yenye damu au nyeusi?

Jiulize!

Je, ninahisi tumbo linajaa mapema au kushiba kwa haraka baada ya kula chakula kidogo tu?

Je, kama natapika damu?
shida ni nini?

Kutapika damu kunaweza kuwa na sababu kadha wa kadha ambazo zinaweza sababisha michubuko katika mfumo huu wa chakula.

sababu hizo ni kama ifuatavyo;

 • Vidonda vya tumbo,
 • Kupasuka kwa mishipa ya koo la chakula,
 • kumeza kitu zaidi ya chakula kinachokwangua koo,
 • Unywaji wa vinywaji vikali,
 • kuingiziwa vifaa katika koo mfano hospitalini,
 • Magonjwa ya damu ya kurithi.

Baadhi ya mambo yanayoweza kuchangia katika kupelekea kutapika damu katika maisha ya kila siku tunayoishi  ni kama yafuatayo;

 1. Historia ya kutapika damu zamani,
 2. Matumizi ya dawa kama Aspirini kwa muda mrefu,
 3. magonjwa ya ini kama homa ya ini, ini kusinyaa au kansa ya ini,
 4. Magonjwa katika mishipa ya damu na
 5. Historia ya kutibiwa kwa mionzi,
 6. Historia ya kutapika damu katika familia.
 
Ndani ya masaa haya kipimo cha kuangalia njia ya mmengenyo kinatakiwa kifanyike kwa watu wenye kutokwa damu inayoendelea.
Idadi ya watu au zaidi wanaoweza kutapika damu kutokana na vidonda vya tumbo.
Asilimia ya watu wanaoacha kutokwa na damu katika mmengenyo wa juu wa chakula itokanayo na vidonda vya tumbo baada ya matibabu.

Jambo la kutambua ni kuwa...

kutapika damu hutokana na shida katika mfumo wa juu wa mmengenyo wa chakula. Muda mwingine unaweza usijue kama unashida katika mfumo huu wa juu wa chakula ambao unahusisha mdomo, umio, tumbo na nusu ya utumbo mdogo. Njia pekee ya kujua kama damu inamwagika ndani bila kutapika ni kuweza kuangalia kinyesi chako kila siku nakuhakikisha hakibadili rangi yake ya kawaida ambayo ni rangi ya kahawia. Rangi ya kinyesi hutofautiana kulingana na chakula unachokula ila ukiona kina rangi nyeusi na kigumu kuflashi basi unaweza jua kama unashida ya kutokwa damu katika mfumo wa juu wa mmengenyo wa chakula.

Mwisho, ukiona unadalili tajwa hapo juu ikiwemo kutapika damu ni vyema ukafika katika kituo cha afya mapema kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Hii  ni kutokana na ukweli kwamba upotezaji wa damu utakaokuwa unaendelea unaweza pelekea kutokufika kwa damu katika ogani za muhimu kama ubongo, figo na maini hivyo kupelekea mwili kuchoka, kupoteza fahamu au kifo cha ghafla.

“Tafadhali onana nasi kabla haujaugua”

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center