Maumivu na muwasho sehemu za siri, tatizo ni nini?

Visababishi hasa ni nini?

Watu wengi wanaume kwa wanawake wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali kwenye sehemu zao za siri kama vile miwasho na maumivu. Matatizo sehemu za siri huathiri utoaji wa mkojo pamoja na mfumo wa uzazi. Watu wengi wanaamini kuwa muwasho sehemu za siri unasababishwa na fangasi tu ila kiuhalisia maumivu na muwasho sehemu za siri inaweza kuwa dalili ya maradhi mbalimbali kama vile magonjwa ya ngozi, magonjwa ya zinaa, minyoo, bawasiri (hemorrhoids) au mzio (allergy).

Kwa wanaume....

Matatizo sehemu za siri za wanaume yanaweza kuwa vidonda, upele, muwasho, maumivu wakati wa kukojoa, maumivu ya korodani, kupungukiwa nguvu za kiume pamoja na matatizo ya uzazi kwa kushindwa kuzalisha mbegu za uzazi. Vyanzo vya matatizo haya ni vingi ikiwemo magojwa ya ngono, magonjwa ya ngozi, yutiai, makovu katika njia ya mkojo yanayosababisha mkojo utoke kwa shida pamoja na saratani ta tezi dume.

Kwa wanawake....

Kama ilivyo kwa mwanaume, mwanamke naye huweza kupata muwasho, maumivu, vidonda au vipele sehemu za siri. Pia, kutokana na magonjwa ya zinaa huweza kutokwa na uchafu ukeni ukiambatana na muwasho na harufu. Vilevile huweza kupata maumivu hasa baada ya tendo la ndoa.

Sambamba na聽 magonjwa ya zinaa, kuwepo kwa chawa, maambukizizi ya bakteria, ugonjwa wa upele (scabies) na allergy; maradhi ya fangasi husababisha muwasho kwa watu wengi ingawa fangasi hushambulia jinsia zote, jinsia ya kike hushambuliwa Zaidi kutokana na maumbile yao ya siri kuwa na unyevunyevu.

Mtu anapataje fangasi sehemu za siri?

聽聽Matumizi ya dawa za antibayotiki kwa muda mrefu bila kufata ushauri wa daktari hali inayopelekea kuua wadudu wanaolinda mwili na kuacha sehemu za siri kukiwa hakuna kinga

聽聽Unene kupita kiasi hivyo kusababisha jasho sehemu za siri na kuongeza unyevunyevu na michubuko.

聽聽Magonjwa yanayosababisha kupungua kwa kinga ya mwili kama vile ukimwi hivyo kupelekea maambukizi ya fangasi kwa urahisi

聽聽Kuwepo na joto kupita kiasi na kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka

聽 聽 聽聽Kuchangia nguo au vifaa vya kuogea na kujamiiana na mru mwenye ugonjwa wa fangas

4 thoughts on “Maumivu na muwasho sehemu za siri, tatizo ni nini?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center