JINSI YA KUMNYOSHESHA MTOTO

Je, wafahamu namna nzuri ya kumnyonyesha mtoto!?

Kumnyonyesha mtoto ย ni jambo la muhimu sana kwa sababu ya faida zake nyingi zikiwemo;

  1. kumkinga mtoto na magonjwa,
  2. kuimarisha Kinga yake ya mwili ,
  3. hujenga uhusiano mkubwa wa upendo kati ya mtoto na mama na faida zingine nyingi.

Namna mtoto anavyowekwa kwenye ziwa la mama, yafuatayo ni muhimu,

  1. Sehemu nyeusi ya chuchu ionekane juu ya mdomo wa mtoto
  2. Mdomo wa mtoto ufunguke vizuri
  3. Kidevu Cha mtoto kiguse ziwa la mama
  4. Namna mama anavyombeba mtoto wakati wa kunyonya, yafuatayo ni muhimu,
  5. Mtoto abebwe karibu na ziwa la mama
  6. Mama atazame ziwa wakati anamnyonyesha mtoto
  7. Mama awe na sehemu ya kuegamia ili mwili wake unyooke wakati ananyonyesha

Umuhimu wa mtoto kunyonya ndani ya muda elekezi

Kwa afya nzuri ya mtoto,inatakiwa anyonye kwa miezi sita ya kwanza bila kulishwa chakula kingine chochote. Hii huwa ngumu kwa siku hizi lakini ni muhimu kwa wamama wote kufahamu faida za kunyonyesha na kuzingatia hili.

Lengo kuu la kunyonyesha

Zaidi ya hayo, mtoto anaponyonya inatakiwa ashibe vizuri na apate maziwa kutoka kwa mama vizuri. Hii itafanikiwa iwapo mama anambeba mtoto vizuri anapomnyonyesha,hii ikijumuisha mtoto anavyokuwa kwenye ziwa la mama na vile hasa mama anavyokuwa amembeba.

Privacy Preference Center