MAZINGIRA YAKO YA KAZI YANAATHIRI VIPI AFYA YAKO?

Ajira zetu zina mchango mkubwa sana  katika maisha yetu kwani asilimia kubwa ya muda hutumika tukiwa kazini ili kuzidi kujistawisha .

Zifahamu athari mbalimbali zinaoweza kuhatarisha afya yako uwapo kazini

  • Kukaa kwenye kiti kwa muda mrefu

Miili yetu inahitaji mazoezi madogo ya mara kwa mara kama kutembea hapa na pale, kwani ndivyo unavyozidi kuiimarisha na kufanya mzunguko wa damu uende ipasavyo.Kukaa kwa muda mrefu huchochea magonjwa kama vile ya moyo,kisukari,kuvimba kwa miguu,kuongezeka kwa uzito, bila kusahau maumivu ya mgongo

  • Matumizi ya teknolojia

Ni kweli kwamba ufanisi wa kazi umeongezeka kwa kiwango kikubwa kupitia teknolojia,vilevile matumizi hayo huweza kutuletea madhara mbalimbali kama vile matatizo ya macho kwa kutumia kompyuta kwa muda mrefu,matatizo ya maskio kwa sauti za kelele za mashine kwa kiwandani

 

  • Kufanya kazi zaidi ya uwezo wako

Binadamu yeyote anahitaji muda wa mapumziko ,ambao utasaidia ubongo kuweza kujiandaa na kuwa na nguvu na kasi  zaidi katika kazi nyingine itakayo fuata.

  • Kutokula mlo kamili na kwa wakati

Ni kweli kwamba mazingira yetu ya kazi hayatupi fursa ya kula chakula muda unaotakiwa la hasha hutupelekea kula vyakula ambavyo ni vya haraka na visivyo vya afya ili kutopoteza mda,hii hupelekea kupata magonjwa ya vidonda vya tumbo pale tunapochelewa kula chakula na magonjwa kama vile ya moyo tunapokula vyakula vya haraka na  vyenye mafuta mengi.

 

  • Mahusiano mabovu na wafanyakazi wengine

kisaikolojia binadamu huwa na afya bora kiakili na kimwili endapo atakuwa na mahusiano mazuri na wanaomzunguka.Mahusiano mabovu hukosesha raha na amani kazini vilevile huchochea usongo wa mawazo na hivyo kuathiri afya  kwa ujumla.

1 thought on “MAZINGIRA YAKO YA KAZI YANAATHIRI VIPI AFYA YAKO?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center